AZILAANI VURUGU HIZO NA KUZIKEMEA
AWATAKA CUF KUHESHIMU MAHAKAMA
Na. Mwandishi wetu.
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amelaani
na kukemea vikali vurugu zilizotokea miongoni mwa wananchama na viongozi wa
chama cha wananchi CUF zilizowahusisha pia baadhi ya waandishi wa habari
walioitikia wito uliotolewa kwao.
Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi katika Picha ya Maktaba.
Taarifa iliyosainiwa na msajili huyo na kusambazwa kwa
vyombo vya habari inasema kuwa msajili huyo anavitaka vyombo vya ulinzi na
usalama katika nchi kulifanyia kazi tukio hilo ili wahusika wafahamike na
kuchukuliwa hatua mara moja, ‘’ninaomba vyombo vya ulinzi na usalama katika
nchi yetu kulifanyia kazi tuio hilo ili wahusika wafahamike na kuchukuliwa
hatua za kisheria’’. Imesema taarifa hiyo,
Aidha msajili Mutungi amesema kuwa vurugu hizo zilionekana
kuvunja Amani na utulivu na watu kuumizwa jambo ambalo ni tofauti na tunu za
taifa za Amani na utulivu huku akiwaasa wanachama wa chama hicho kuwa pamoja na
tofauti walizonazo kutulia kusubiri uamuzi wa mahakama kwa kuwa tayari suala
hilo liko mahakamani.
‘’ni ukweli usiopingika kuwa suala la mgogoro wa uongozi
katika chama cha CUF lipo mahakamani, lakini nikiwa msimamizi wa sheria ya
vyama vya siasa na kutambuliwa na kutambuliwa na jamii na jamii kuwa ni mlezi
wa vyama vya siasa, nimelazimika kuwasihi wadau wa siasa hususani wanachama wa
chama cha CUF, kutambua kwamba kuwapo kwa shauri mahakamani siyo fursa ya
kufanya vitendo vya uvunjifu wa Amani, kwani kwani jambo hili ni uvunjifu wa
sheria na linaleta sura mbaya kwa jamii’’. Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo.
Jaji Mutungi akiwa na Malim Seif
Hayo yamejili ikiwa juzi tarehe 22 mwezi huu wa nne, akiwa
katika mkutano na waandishi wa habari uliotishwa na mwenyekiti wa chama cha
wananchi CUF wilaya ya Kinondoni bwana Juma Mkumbi ambaye pia ni mjumbe wa
baraza kuu la uongozi la taifa la chama hicho anayedaiwa kumuunga mkono katibu
mkuu wa maalim seif sharrif Hamad kuvamiwa na watu wasiojulikana wanaozaniwa
kuwa ni wafuasi wa mwenyekiti wa chama hicho profesa Ibrahim Lipumba na
kuvuruga mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya VINA iliyopo Mabibo Farasi
jijini Dar es salaam.
Katika tukio hilo watu kadhaa walijeruhiwa ikiwemo waandishi
wa habari na mmoja wa waliovamia kiasi cha kushambuliwa na wananchi wenye
hasira kali mpaka alipookolewa na polisi na kupelekwa katika kituo cha polisi
magomeni.