WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Friday, July 21, 2017

HIVI NDIVYO MORINYO ALIVYOMZIDI GUADIOLA

Manchester United imejipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester City katika debi ya kwanza ugenini huku ziara za 2017 zinazofadhiliwa na Aon zikiendelea kuipatia ushindi the red Devils.
 Romelu Lukaku na Marcus Rashford wakisherehekea ushindi wa mabao yao
 Romelu Lukaku na Marcus Rashford wakisherehekea ushindi wa mabao yao

Romelu Lukaku na Marcus Rashford waliisaidia United katika mabao yote mawili yaliofungwa katika kipindi cha kwanza.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho kilianza kwa mashambulizi huku Anders Herrera akianzisha juhudi hizo mapema, huku mashambulio mengine yakitoka nje ya eneo la hatari ,United wakimjaribu kipa mpya wa City Ederson.

David De Gea alilazimika kuwa macho katika upande mwengine huku Raheem Sterling akishambulia mara mbili , kabla ya Chris Smalling kuzuia mashambulizi mawili yaliofanywa na Patrick Roberts na Sterling.

United hatahivyo ilifanikiwa dakika nane kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza baada ya Lukaku kupata pasi muruwa kutoka kwa Paul Pogba na kucheka na wavu.
Dakika mbili baadaye Marcus Rashford aliifungia United bao la pili akifunga baada ya kazi nzuri kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan

BREAKING NEWS:- Msemaji wa mawakili wa Trump ajiuzulu

Rais TrumpRais Trump 
Msemaji wa mawakili wa rais Donald Trump amejiuzulu, kulingana na vyombo vya habari.
Mark Corallo alikuwa msemaji wa Marc Kasowitz ambaye anamtetea Trump katika uchunguzi kuhusu Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani na kumsaidia rais huyo kupata ushindi.
Ripoti zinasema kuwa bwana Corallo alitofautiana na mipango ya mawakili wa Trump kuwadharau na hata kupunguza uwezo wa maafisa wanaoongoza uchunguzi huo.

Hakujakuwa na tamko lolote kutoka kwake ama hata mawakili hao wa Trump.
Bwana Corallo ni mwandani wa wakili wa idara ya haki Robert Mueller ambaye anaongoza uchunguzi huo dhidi ya Urusi na amemsifu hadharani kulingana na mtandao wa politico.
Afisa huyo amekatishwa tamaa na operesheni za mawakili hao mbali na kambi pinzani zilizopo, ripoti hiyo imeongezea.

Bwana Mueller amewaajiri watu maarufu kujiunga na kundi lake, ambalo linachunguza iwapo kulikuwa na ushirikiano wowote kutoka kwa kundi la Trump ambao Urusi na rais Trump amekana kuwepo.

UTALII : Taifa la Tanzania latajwa kuwa eneo bora la Safari Afrika

Safari katika mbunga ya Serengeti nchini Tanzania 
Safari katika mbunga ya Serengeti nchini Tanzania


Taifa la Tanzania limetajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii barani Afrika kulingana na mtandao wa SafaricBookings.com ambao ndio mtandao mkubwa wa ukuzaji wa safari za Afrika.
Mtandao huo ulifanya tathmini ya zaidi ya wataalam 2500 na wale walioshiriki katika safari hizo kabla ya kutangaza kuwa Tanzania ndio eneo bora la safari mwaka 2017.

Tathmini hizo ziliandikwa na watalii walioenda safari pamoja na wataalam bingwa wa Afrika.
Mtandao huo unasema kuwa uchanganuzi huo pia ulibaini kwamba Tanzania ilipata umaarufu wake kutokana na idadi ya wanyama mbali mbali.

Watu maarufu katika miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakizuru taifa hilo wakitembelea maeneo tofauti ya vivutio vya utalii nchini Tanzania.

Watu hao ni mwanamuziki maarufu Usher Raymond, aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United na Real Madrid David Beckham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho , mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin na nyota wa filamu kutoka Marekani Will Smith na Harrison Ford.

Walitembelea mbuga za Serengeti na mlima kilimanjaro.
Mtandao huo uliitaja Zambia kuwa taifa lenye kivutio kizuri cha misitu huku wataalam wote wakikubaliana kwamba mazingira ya misitu nchini humo mi mazuri zaidi.
Vilevile Zambia pia ilitajwa kuwa taifa lenye maisha bora ya ndege.
Namibia na Kenya zilitajwa kuwa bora katika mandhari mazuri pamoja na ndege waliopo mtawalia.

WAKATI NKURUNZINZA AKIWAKARIBISHA NYUMBANI WARUNDI WAZAMIA MAREKANI

Vijana sita wa Burundi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya roboti nchini Marekani wameripotiwa kutoweka, polisi wanasema.

Vijana sita wa Burundi waliotoweka katika mashindano ya roboti nchini Marekani

Wavulana wanne na wasichana 2 walio kati ya umri wa miaka 16 na 18 walipotea wakati wa mashindano hayo ya kwanza duniani yaliofanyika Washington DC.
Idara ya polisi mjini humo imesema kuwa mara ya mwisho vijana hao kuonekana ilikuwa siku ya Jumanne wakati wa makamilisho ya michezo hiyo.
Ripoti zinasema kuwa vijana wawili kati yao tayari wamevuka mpaka na kuingia Canada lakini ripoti hiyo haijathibitishwa na polisi.

Siku ya Alhamisi, idara ya polisi mjini humo ilibandika picha za sura za vijana hao sita waliopotea katika mtandao wao wa Twitter, wakiwataka raia kuwasiliana nao iwapo watakuwa na habari yoyote kuwahusu.
Vijana hao wanatambulika kuwa Don Ingabire, Kevin Sambukiza, Nice Munezero, Audry Mwamikazi, Richard Irakoze na Aristide Irambona.
Waandalizi wa mashindano hayo wanasema kuwa waliwaeleza polisi baada ya msimamizi wa timu hiyo ya Burundi kushindwa kuwapata vijana hao.
Katika taarifa , msemaji wa mashindano hayo Jose Escotto alisema, ripoti kamili imewasilishwa kwa polisi ambao wanachunguza kisa hicho, kulingana na gazeti la The Washington Post.

Mashindano hayo ya siku 3 yalihudhuriwa na timu 150 zilizokuwa zikishindana.
Mashindano hayo yanalenga kuwashawishi vijana kukuza vipaji vyao katika masomo ya sayansi, technolojia, uhandisi na hesabu.

Monday, July 17, 2017

BREAKING NEWS:- MSAJILI JAJI MUTUNGI ASHUSHA RUNGU ZITO KWA VYAMA VYA SIASA

  • sasa Ripoti ya CAG Kuwakaanga
  • vyatakiwa kutaja vyanzo vya mapato vya nje na ndani
  • waliofuja Ruzuku kukiona cha moto
  • TCD nayo kueleza matumizi ya gawio la Serikali

Na. Mwandishi Wetu

Upepo wa kusimamia Rasilimali za nchi, kubana matumizi na kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha zinazotokana na kodi ya watanzania sasa umezidi kushika kasi katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inayoongozwa na Jaji Fransis Mutungi.

uchunguzi uliofanywa na JAMVI LA HABARI, unaonyesha kwamba Tayari Msajili wa vyama vya siasa amevilima barua vyama vyote vya siasa hapa nchini vinavyopokea ruzuku na kuvipatia maelekezo kadhaa ya utekelezaji haraka iwezekanavyo.

Chanzo chetu cha siri kilichopo ndani ya chama kimoja cha siasa kikubwa hapa nchini kimedokeza kuwa tayari wao kama chama wameshasikia tetesi za kupewa maelekezo ya kiusimamizi wa fedha na kwamba kwa sasa wanasubiri barua rasmi kutoka ofisi hiyo.

"Mpaka sasa hatujapokea barua bado lakini tumesikia chinichini kwamba tunawindwa". Kimenukuliwa chanzo chetu hicho

Taarifa za uhakika zinasema kuwa moja ya mambo ambayo msajili na ofisi yake wanataka vyama vya siasa vifanye haraka iwezekanavyo ni pamoja na utekelezaji wa maelekezo aliyowapa awali ya kuvitaka vyama hivyo kutengenisha akaunti za kupokea fedha za ruzuku na michango ama vyanzo vingine ili kudhibiti matumizi ya ruzuku ambazo ni fedha zinazotokana na kodi za watanzania.

Aidha Msajili anadaiwa kuvielekeza vyama vyote vya siasa kuweka hadharani vyanzo vyao vyote halali vya mapato tofauti na ruzuku na kuwafahamisha wanachama wao jambo ambalo linapongezwa kuwa ni njia sahihi kudhibiti matumizi ya fedha haramu katika vyama vya siasa 

" unajua vyama vya siasa ni taasisi za umma, lakini vimekuwa vikipokea mamilioni ya fedha safi na chafu bila kutoa taarifa na kujikuta vikitumika kuhalalisha fedha haramu". Anasema  Saidi Kambi wa Chuo cha  Diplomasia alipoulizwa kuhusu jambo hilo.

Mwaka 2013 Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG ilisema kwamba vyama vyote vya siasa havikaguliwi japo vinapokea fedha za ruzuku na kuzua mjadala uliopelekea vyama hivyo kuanza kukaguliwa.

Sheria namna saba  ya uanzishwaji wa vyama vya siasa ya mwaka 1992 inamtaja msajili wa vyama vya siasa kama msajili, mlezi na mtunza kumbukumbu wa vyama vyote vya siasa vilivyopo hapa nchini na aliyepewa mamlaka ya kuvipatia ruzuku kwa mujibu wa sheria na hata kuvifuta vyama hivyo iwapo havitakidhi matakwa ya kisheria ya kuanzishwa kwao.
 
mbali na vyama vya siasa, pia kituo cha demokrasia Tanzania kinachoundwa na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni TCD (Tanzania Center for Democracy) ni miongoni wa taasisi zitakazokumbwa na mchakato huu.

Kitendo cha msajili Mutungi kuanzisha mchakato huu wa ukaguzi wa fedha za vyama vya siasa kimekuja wakati tayari kukiwa na Malalamiko kadhaa ya baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama kuhusu ufujaji wa fedha zinazotokana na ruzuku ikiwemo kulipana mishahara na madeni hewa baina ya viongozi jambo ambalo haliruhusiwi kisheria.

Jamvi la Habari litaendelea kuwajuza kila hatua kuhusiana na jambo hili muhimu.