- sasa Ripoti ya CAG Kuwakaanga
- vyatakiwa kutaja vyanzo vya mapato vya nje na ndani
- waliofuja Ruzuku kukiona cha moto
- TCD nayo kueleza matumizi ya gawio la Serikali
Na. Mwandishi Wetu
Upepo
wa kusimamia Rasilimali za nchi, kubana matumizi na kuhakikisha
matumizi sahihi ya fedha zinazotokana na kodi ya watanzania sasa umezidi
kushika kasi katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inayoongozwa na
Jaji Fransis Mutungi.
uchunguzi
uliofanywa na JAMVI LA HABARI, unaonyesha kwamba Tayari Msajili wa
vyama vya siasa amevilima barua vyama vyote vya siasa hapa nchini
vinavyopokea ruzuku na kuvipatia maelekezo kadhaa ya utekelezaji haraka
iwezekanavyo.
Chanzo
chetu cha siri kilichopo ndani ya chama kimoja cha siasa kikubwa hapa
nchini kimedokeza kuwa tayari wao kama chama wameshasikia tetesi za
kupewa maelekezo ya kiusimamizi wa fedha na kwamba kwa sasa wanasubiri
barua rasmi kutoka ofisi hiyo.
"Mpaka sasa hatujapokea barua bado lakini tumesikia chinichini kwamba tunawindwa". Kimenukuliwa chanzo chetu hicho
Taarifa
za uhakika zinasema kuwa moja ya mambo ambayo msajili na ofisi yake
wanataka vyama vya siasa vifanye haraka iwezekanavyo ni pamoja na
utekelezaji wa maelekezo aliyowapa awali ya kuvitaka vyama hivyo
kutengenisha akaunti za kupokea fedha za ruzuku na michango ama vyanzo
vingine ili kudhibiti matumizi ya ruzuku ambazo ni fedha zinazotokana na
kodi za watanzania.
Aidha
Msajili anadaiwa kuvielekeza vyama vyote vya siasa kuweka hadharani
vyanzo vyao vyote halali vya mapato tofauti na ruzuku na kuwafahamisha
wanachama wao jambo ambalo linapongezwa kuwa ni njia sahihi kudhibiti
matumizi ya fedha haramu katika vyama vya siasa
"
unajua vyama vya siasa ni taasisi za umma, lakini vimekuwa vikipokea
mamilioni ya fedha safi na chafu bila kutoa taarifa na kujikuta
vikitumika kuhalalisha fedha haramu". Anasema Saidi Kambi wa Chuo cha
Diplomasia alipoulizwa kuhusu jambo hilo.
Mwaka
2013 Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG
ilisema kwamba vyama vyote vya siasa havikaguliwi japo vinapokea fedha
za ruzuku na kuzua mjadala uliopelekea vyama hivyo kuanza kukaguliwa.
Sheria
namna saba ya uanzishwaji wa vyama vya siasa ya mwaka 1992 inamtaja
msajili wa vyama vya siasa kama msajili, mlezi na mtunza kumbukumbu wa
vyama vyote vya siasa vilivyopo hapa nchini na aliyepewa mamlaka ya
kuvipatia ruzuku kwa mujibu wa sheria na hata kuvifuta vyama hivyo iwapo
havitakidhi matakwa ya kisheria ya kuanzishwa kwao.
mbali na vyama vya siasa, pia kituo cha demokrasia Tanzania kinachoundwa na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni TCD (Tanzania Center for Democracy) ni miongoni wa taasisi zitakazokumbwa na mchakato huu.
Kitendo
cha msajili Mutungi kuanzisha mchakato huu wa ukaguzi wa fedha za vyama
vya siasa kimekuja wakati tayari kukiwa na Malalamiko kadhaa ya baadhi
ya viongozi na wanachama wa vyama kuhusu ufujaji wa fedha zinazotokana
na ruzuku ikiwemo kulipana mishahara na madeni hewa baina ya viongozi
jambo ambalo haliruhusiwi kisheria.
Jamvi la Habari litaendelea kuwajuza kila hatua kuhusiana na jambo hili muhimu.
No comments:
Post a Comment