Na Ibrahim malinda
IKIWA jana Oktoba 25, imetimia miaka miwili,
tangu watanzania wapige kura za Uchaguzi Mkuu na kuchagua Rais, wabunge
na Madiwani ambapo Dk. John Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa tano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mageuzi makubwa yameelezwa kufanyika
katika sekta mbalimbali za kimaendeleo kwa kipindi cha miaka miwili ya
uongozi wake imeelezwa.
Mageuzi hayo ni pamoja na kufanikisha
elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, ambapo hivi sasa
wanafunzi wanagharamiwa kila kitu na serikali kuanzia ada za shule,
mitihani, chakula, jambo ambalo kwa miaka zaidi ya 20, halikuwepo.
Kuwezekana
kwa jambo hilo, kumemfanya Dk. Magufuli kuwa mmoja wa viongozi hodari
walioweza kutimiza ahadi zao ndani ya muda mfupi na hata kutoa taswira
kubwa ya mabadiliko ya maendeleo ambayo kwa namna moja au nyingine
walikuwa hakuna.
Taarifa ilizozipata gazeti hili, zilieleza kuwa
elimu bora imekuwa mkombozi na hata kufanya kila mzazi kupunguziwa
majukumu ya masomo kwa watoto, ambao awali ilikuwa mtihani mkubwa kwa
wananchi kushindwa kumudu gharama za masomo.
Mmoja wa mwananchi
aliyezungumza na gazeti hili, Joseph Yona, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
CCM wa Tawi la Bokorani, lililopo Temeke, alisema kuwezekana kwa elimu
bure ni msaada tosha kwa wananchi, ambao kwa muda mrefu walikuwa
wanashindwa kusomesha watoto wao.
“Elimu ni nyenzo ya maendeleo,
anapojitokeza kiongozi anaweka jitihada kubwa katika elimu ni msaada
tosha. Naifurahia kura yangu niliyoipiga kwa kuwa imesaidia kupata
kiongozi bora na mwenye malengo makubwa kwa nchi,’’alisema alipokuwa
anazungumza na gazeti hili.
Jamvi la Habari, lilielezwa kuwa
ununuzi wa ndege sita mpya , ni uamuzi ambao unatajwa ni wa kihistoria,
ambapo kwa muda mrefu nchi ilikosa ndege zake na hata kuhatarisha ustawi
wa Shirika la Ndege Tanzania(ATCL), ambalo lilikuwa linaelekea kuzimu.
Kuzinduka
kwa shirika la ndege ni moja ya hatua kubwa ya kukuza mapato kwa taifa
lolote, hivyo inaelezwa uwepo wa ndege hizo ni hatua kubwa ya
kimaendeleo, ambayo kila mtanzania anapaswa kufurahia maendeleo hayo,
ambayo yamekuwa makubwa sana.
Akizungumzia fursa za uwepo wa
ndege hizo, mfanyabiashara Yusuph Rashid alisema nchi kuwa na ndege zake
ni hatua kubwa, hivyo kila mtanzania anapaswa kuona hii ni ufahari
mkubwa ambao nchi itapata maendeleo makubwa.
“Leo hii soko la
ndege ya Afrika kwa nchi za Afrika limetekwa na Kenya, pamoja na
Ethiopia, hivyo nasi lazima tuwe na uhakika wa ndege zetu kwa vile
Tanzania inaouwezo mkubwa wa kuwa na mashirika makubwa ya ndege, ambayo
kwa namna moja au nyingine tunaouwezo huo,’’alisema.
Taarifa
zaidi ilieleza kuwa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha stardand
gauge kutoka Dar es Salaam hadi, Mwanza na Kigoma ni hatua moja kubwa ya
kimaendeleo, ambapo kwa zaidi ya miaka 100 reli mpya ya kisasa ilikuwa
hakuna, hivyo uwepo wa reli hiyo ni hatua moja kubwa ya kimaendeleo.
Ujenzi
wa Barabara za Juu Ubungo na makutano ya Tazara, ni fursa kubwa ya
ujenzi wa uchumi imara, ambayo Rais Dk. Magufuli amenuia kuiletea sifa
kubwa nchi, kutokana na uwepo wa maendeleo hayo ni hatua moja kubwa ya
kimaendeleo kwa nchi kusonga mbele.
Jamvi la Habari linaeleza
kuwa uwepo wa mabadiliko makubwa ya kisheria katika sekta ya madini na
nchi kuanza kunufaika na mabadiliko hayo, ni hatua kubwa ya kimaendeleo
na hata kila mmoja kuona kuwa ufahari mkubwa wa ulinzi wa rasilimali za
nchi kuwa zinalindwa kwa kiasi kikubwa.
Pia, inaelezwa katika
kipindi cha miaka miwili Rais Dk. Magufuli ameweza kunipa heshima nchi
kwa kuhakikisha tunalipwa zaidi ya Bilioni 700 na kampuni ya ACCACIA
kutokana na kukwepa kodi.
Uwezekano wa jambo hilo ndio unafanya
kuwepo kwa maendeleo makubwa ya nchi yanakuja ndani ya kipindi cha miaka
mitano ya utawala wa Rais Magufuli kufanikiwa hasa kutokana na mapato
ya kila mwezi kupanda maradufu.
Taarifa za Mamlaka ya
Mapato(TRA), zinaeleza kuwa mapato ya nchi kila mwaka yanapanda ambapo
sasa hivi kila mwezi toka utawala wa Dk. Magufuli, mapato yamefikia sh.
Trilioni 1.3 tofauti na awali ilikuwa bilioni 900.
Ujenzi Bomba
la Mafuta Kutoka Uganda Mpaka Tanga, ni mradi mkubwa unaotajwa kuwa na
mafanikio makubwa kwenye utawala wa Rais Magufuli kwa kuwa utaweza
kutengeneza ajira zaidi ya milioni mbili pamoja na kuipa mapato makubwa
nchi.
Uwezekano wa mradi huo, ambao unatajwa kuwa moja ya miradi
mikubwa kufanyika nchini, unazidi kueleza mafanikio ya utawala wa Rais
Dk. Magufuli kuwa utakuwa salama na maendeleo makubwa kwa nchi.
Pia,
inaelezwa udhibiti wa fedha za umma, unazidi kumpa heshima Rais Dk.
Magufuli kutokana na aina ya utawala wake kuheshimu fedha za wananchi
katika utekelezaji wa miradi mbali mbali nchini.
Jamvi la Habari
lilielezwa kuwa ifikapo 2020 zaidi ya asilimia 95, mijini na vijini
kutakuwa na uhakika wa maji safi na salama kutokana na utekelezaji wa
miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za ndani pamoja na wahisani
waliolizika na utawala imara wa Rais Dk. Magufuli.
Katika kipindi
cha miaka miwili ya Rais Dk. Magufuli huduma mbalimbali za afya
zimeboreshwa ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba na huduma kama, MRI, CT-SCAN
zanunuliwa kwa mafanikio makubwa.
Pia Rais Magufuli amefanikiwa
kudhibiti upotevu wa Mapato Bandarin pamoja na kufanikiwa kuimarisha
miundombinu ya barabara sehemu mbali mbali ya nchi.
No comments:
Post a Comment