WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Saturday, October 1, 2016

MAPAMBANO : Urusi yapeleka ndege zaidi nchini Syria

DW.
Urusi inapeleka ndege zaidi nchini Syria kuimarisha operesheni zake za angani, limeripoti gazeti la nchini Urusi. Haya yanajiri Marekani ikisema juhudi za kidiplomasia kuumaliza mzozo wa Syria ziko katika 'hali mahtuti'.

default

Gazeti la Izvestia limeandika kwamba  ndege kadhaa chapa Su-24 na Su-34 zimewasili katika kituo cha anga cha Hmeymin nchini Syria.

Wakati huo huo Urusi imekanusha taarifa kwamba operesheni zake ndani ya Syria ambazo sasa zimetimiza mwaka mmoja, zimewauwa watu 10,000. Taarifa hiyo ilitolewa jana na shirika la kuchunguza haki za binadamu nchini Syria lililo na makao yake nchini Uingereza.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Kremlin Dmitry Peskov, amesema hawaichukulii taarifa ya ofisi zake nchini Uingereza kuwa ya kuaminika. Kwa mujibu wa shirika hilo la uchunguzi, watoto 900 ni miongoni mwa wahanga wa mashambulizi ya Urusi.

Mabomu yazidi kurindima Aleppo

Mapigano yanaendelea katika kampeni ya wiki nzima ya serikali ya Syria inayosaidiwa na Urusi, ikilenga kuwatimua wapinzani Mashariki mwa mji huo, eneo la mwisho la mjini linaloshikiliwa na waasi wa serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Urusi na serikali ya Assad waliutupilia mbali mpango wa kusitisha mapigano uliokuwa umefikiwa kati ya Marekani na Urusi mwezi uliopita, na kuanzisha operesheni dhidi ya waasi Mashariki mwa Aleppo, inayoonekana kuwa kubwa zaidi tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wamefanya mazungumzo ya simu kwa siku ya tatu mfululizo. Baadaye Lavrov amesema nchi yake ingekuwa tayari kufikiria njia zaidi ya moja ya kurejesha utulivu mjini Aleppo.

Lavrov hata hivyo ameikosoa Marekani kwa kushindwa kuwatenganisha waasi wenye misimamo laini na wale ambao Urusi inawaita magaidi, hali ambayo Urusi inasema ililiwezesha kundi ambalo siku za nyuma lilijulikana kama al-Nusra Front kuyakiuka makubaliano ya kusitisha uhasama yaliyofikiwa kati ya Marekani na Urusi tarehe 9 Septemba.

Msimamo wa Marekani njia panda

Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Urusi, John Kerry (kushoto) na Sergei Lavrov (kulia)
Ijumaa Marekani ilisema bayana kuwa haijawa tayari kuitekeleza hatua ya kusitisha ushirikiano na Urusi, iliyokuwa imeitangaza ikiwa Urusi isingechukua hatua za haraka kusimamisha ghasia mjini Aleppo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Mark Toner  amesema bado makubaliano ya amani hayajafa kabisa, na kuongeza kuwa wasingependa kuona mlango wa kidiplomasia ukifungwa kabisa.
Katika mazungumzo ya wanaharakati wa Syria pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, John Kerry aliwaambia wanaharakati hao kuwa utawala wa rais Obama umeshindwa kutoa kitisho chhochote cha kijeshi, ambacho kingezipa nguvu hoja zake katika mazungumzo yake na Urusi.

''Nadhani kuna watu watatu au wanne ndani ya utawala huo wanaopigia debe matumizi ya nguvu za kijeshi, na nimeshindwa '', waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amenukuliwa na gazeti la New York Times akiwaambia wasyria hao.

KENYATA AVUNJA REKODI: AGAWA LAPTOP KWA WANAFUNZI WOTE KENYA

http://www.newvision.co.ug/w-images/a6e8a133-de98-4d43-9f72-928a308dca0d/2/KENYATA-703x422.jpg                                                 Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

 http://gdb.voanews.com/09EAFEED-D17C-4DAE-A3E6-D6214836E938_w987_r1_s.jpg            Wanafunzi wakiwa darasani kwenye shule ya Youth for Technology Foundation mjini Nairobi


Katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutimiza na kutekeleza ahadi zake kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao, Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, imetangaza rasmi kuanza kuwapa wanafunzi wote wa shule za msingi za umma nchini humo vipakatalishi, yaani laptop kuanzia Ijumaa Septemba 30 na litakamilika katika kipindi cha mwezi mmoja.

Mara tu baada ya kuchaguliwa mwaka 2013, Rais Kenyatta aliahidi kuyafanya masomo kuwa kwenye mfumo wa kidigitali kwa kuwapa wanafunzi wote wa shule za umma nchini humo vipakatalishi hivyo.

Likiwa ni zoezi lililotarajiwa kwa hamu kubwa kote nchini, serikali hatimaye imeanza mchakato wa kuwapa wanafunzi wa shule za msingi za umma vipakatalishi vitakavyowawezesha kufuatilia masomo katika mfumo wa kidigitali. Japo zoezi hili halijafika wakati alioutangaza Rais, serikali yake imekuwa mbioni kuhakikisha kuwa ahadi muhimu alizozitoa mara tu baada ya kuchaguliwa kwake zinatimizwa.

Waziri wa Elimu nchini humo, Fred Matiang’i anasema kuwa vipakatalishi hivyo vimeundwa kwa mtaala wa kisasa na hivyo basi utawawezesha wanafunzi na shule za umma kuukumbatia mfumo wa kidigitali unaokumbatiwa na mataifa yaliyoendelea. Bwana Matiang’i akiahidi kutoa tangazo la kuidhinishwa kwa mtaala mpya wa mafunzo kwa walimu kote nchini.

Naye waziri wa Sayansi na Teknolojia, Joe Mucheru aanasema kuwa serikali tayari imewapa mafunzo ya kutosha walimu watakaobeba jukumu la kuwaongoza wanafunzi kote nchini kupata mafunzo muhimu jinsi ilivyo katika mtaala.

Suala ambalo limeonekana kuwa tete ni iwapo shule za msingi za umma takriban milioni moja nukta mbili zimejengewa miundo msingi inayofaa kama vile umeme. Waziri wa Kawi Charles Keter anaeleza kuwa shule zote zitakuwa na umeme kabla ya mwaka huu kumalizika.

Zaidi ya vipakatalishi 1,060 tayari vimepokelewa nchini na nyingine zipatao 22,000 zikitarajiwa kufika nchini kila wiki.

china yazindua VYOO VYA KIOO

China imezidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani.

Vyoo hivyo, vimejengwa karibu na Ziwa Shiyan, katika mkoa wa Hunan kusini mwa nchi hiyo.
Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani.
 http://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/25A3/production/_91453690_5a4943a1-3b28-4f12-b5ea-d0436cd907d4.jpg
Aidha, walio nje wanaweza kuona walio ndani ya vyoo.

Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema ni watu wachache sana waliotumia vyoo hivyo siku ya kuzinduliwa kwake.
 http://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/BDFB/production/_91453684_8d07ee37-68ab-4ded-aa61-2d8ae6c29f0f.jpg
Licha ya umaarufu wa mijengo ya kutumia vioo katika ujenzi, hasa kwenye madaraja na barabara, baadhi ya miradi imefungwa.

Kuta za kutenganisha vyoo, hata vile vya wanaume na wanawake, vimetiwa tu ukungu kidogo
Habari za kuzinduliwa kwa vyoo hivyo zimevuma sana.

Ejike Nnadi, akichangia ujumbe wa Facebook wa runinga ya taifa CCTV amesema: "Hapana".
Lakini kunao wengine wanaosema wanaweza kujaribu kuvitumia.
Tina Chen anasema mradi huo wa vyoo ni ishara kwamba kuna mtu alikuwa na pesa za "kupoteza".
  Kuna njia ya vioo iliyojengwa juu mlimani Tianmen

Jaji mkuu atimuliwa kwa kutotoa vyeti vya ndoa za jinsia moja

http://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/16EC8/production/_91469839_3f408bd2-d06e-4c08-845b-e2639c25c0aa.jpg


Jimbo la Alabama, nchini Marekani, limemwondoa kazini jaji mkuu aliyekaidi uamuzi wa mahakama ya juu kuhusu ndoa za jinsia moja.

Ray Moore aliagiza kwamba wapenzi wa jinsia moja wanyimwe vyeti vya ndoa, hata baada ya uamuzi wa kihistoria mwaka jana, uliohalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Ametaja uamuzi wa kuondolewa kwake kama kampeni ya makundi ya wapenzi wa jinsia moja, ya kuendeleza ajenda iliyo kinyume na maadili.

Kundi la wanaharakati lililompeleka mahakamani linasema kwamba alikabidhiwa wadhfa wake kama jaji mkuu wala sio mchungaji.

Bwana Moore, anafahamika na wengi kwa hatua yake ya kujenga mnara wa amri kumi za Bibilia kwenye majengo ya mahakama ya jimbo hilo, amekuwa akizungumza kwa uwazi dhidi ya ndoa za jinsia moja.
Jaji huyo pia kwa wakati mmoja aliwataka majaji wa jimbo la Alabama kutotoa vyeti vya ndoa kwa wapenzi wa jinsia moja, kinyume na uamuzi wa mahakama ya juu nchini Marekani.

 Ray Moore aliagiza kwamba wapenzi wa jinsia moja wanyimwe vyeti vya ndoa, hata baada ya uamuzi wa kihistoria mwaka jana, uliohalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Maganda ya chungwa yampatia shilingi milioni 100

http://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/5DF3/production/_91415042_orangepeels.jpg

Msichana wa miaka 16 nchini Afrika Kusini amejishindia zawadi ya maonyesho ya Google kwa kutumia maganda ya chungwa kutengeza kifaa kinachosaidia udongo kuhifadhi maji.
Kiara Nirghin aliwashinda wanafunzi wengine duniani kwa kujipatia ufadhili wa masomo wenye thamani ya dola 50,000 kwa ''kukabiliana na kiangazi kupitia chungwa''.
Kazi yake inajiri kufuatia kiangazi ambacho kinaendelea kuathiri Afrika Kusini.

Kiangazi hicho ambacho ni kibaya zaidi kuwahi kutokea tangu 1982 kimeathiri mimea huku mifugo ikifariki.
Kwa sasa anatumai kwamba mbinu hiyo inaweza kuwasaidia wakulima kuhifadhi fedha pamoja na mimea.

Samsung kuuza tena Galaxy Note 7

http://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/D288/production/_91469835_1ac7a429-bc29-4cc5-83e2-b43399fd11e1.jpg
                         aina ya simu ya samsung gallaxy note7 iliyoripuka

http://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/AB78/production/_91469834_31979b0c-d0d0-4cf2-81e5-a483dee47279.jpgTakriban simu, Galaxy Note 7, milioni mbili laki tano zilirejeshwa kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, ili kupata btari mpya. 


Samsung imeanza mauzo ya simu yake, Galaxy Note-Seven nchini korea kusini, baada ya kusitisha mauzo yake mwezi mmoja uliopita, kutokana na madai kwamba simu hizo zinalipuka.
Kampuni hiyo inasema hitilafu kwenye batri zake zilisababisha milipuko hiyo.
Takriban simu milioni mbili laki tano zilirejeshwa kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, ili kupata btari mpya.
Makampuni ya usafiri wa ndege yamekuwa yakiwaonya wateja wake dhidi ya kutumia simu hiyo ndani ya ndege.
Hata hivyo sio simu zote zilizo na hitilafu kwenye batri zilizorejeshwa, na hivyo haijulikani wazi wakati marufuku ya kutumia simu hizo ndani ya ndege itakapoondolewa.
Samsung inatoa simu za bure kwa wale walioathirika huku wafanyibiashara wa simu hizo wakipata mali mpya huku simu zaidi zikiendelea kufikishwa sokoni
''Tumetoa wito kwa waathiriwa wa simu hizo kuzibadilisha haraka iwezekanavyo. Simu ya galaxy Note 7 zenye betri ishara ya betri ya kijani zilikuwa salama kutumia'',Samsung imesema.

Video ya raia wa Uganda akiuwawa na polisi Marekani yatolewa

http://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/A137/production/_91417214_olangoprotest.jpg
 Waandamanaji, akiwemo Bi Agnes Hassan (aliyejifunga kitambaa kichwani), wakilalamikia kuuawa kwa Olango 

Polisi katika mji wa Marekani San Diego wametoa mkanda wa video ya mwanamme mweusi aliyepigwa risasi na kuuwawa na polisi siku ya jumanne.


Video hiyo inaonyesha maafisa wawili wa polisi wakimkaribia Alfred Olango - mkimbizi kutoka Uganda - ambaye hakuwa amejihami, kabla ya mmoja wao kumfyatulia risasi katika mtaa wa El Cajon.
Polisi wanasema kwamba mwanamme huyo alionyesha tabia potovu isiyoeleweka, japo mamake mzazi anasema alikuwa na matatizo ya kiakili na alifaa kupata usaidizi.

Tukio hilo lilisababisha maaandamano makali katika eneo la El Cajon.
Polisi huyo anaonekana akifyatua risasi mara nne, baada ya mwanamme huyo kuinua mikono yake hadi kwenye eneo la kifua, ishara ambayo polisi wanasema ilikuwa ya kujitayarisha kufyatua risasi.
Video hiyo imetolewa baada ya siku tatu za maandamano makali , na katika mkesha wa siku ambayo familia ya mwanamme huyo iliitisha maandamano makubwa.

Familia ya mwanamme huyo ilikuwa ikiwashinikiza polisi kutoa mkanda wa video wa tukio hilo.
Mkuu wa polisi Jeff Davis anasema video hiyo imetolewa ili kutuliza ghadhabu ya umma.

 http://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/EF57/production/_91417216_elcajon.jpg
                                  Polisi wamekiri kwamba Olango hakuwa na silaha

Olango, aliye na umri wa miaka 38, mkimbizi kutoka Uganda ambaye ameishi nchini Marekani tangu utotoni, alipigwa risasi baada ya polisi kujibu ripoti kuhusu mwanamme aliyekuwa na matatizo ya kiakili, ambaye alikuwa akitembea ovyo barabarani.

Polisi wanasema, Olango, alikataa kuondoa mkono wake kwenye mfuko alipioagizwa, na alifyatuliwa risasi baada ya kuondoa kifaa kwenye mfuko, na kufanya ishara ya kufyatua risasi.

Kulingana na polisi, aliwaelekezea kifaa chenye ncha kali "kana kwamba alikuwa anawafyatulia risasi, japo baadaye ikagunduliwa kifaa hicho kilikuwa cha sigareti ya elektroniki.
BBC SWAHILI