WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, January 17, 2018

MAAJABU : Apasuka koo kwa kujaribu kuzuia kupiga chafya

Madaktari wa upasuaji wakimuhudumia mgonjwaMadaktari wameonya kwamba kuzuia kupiga chafya kwa kufunga pua na mdomo kunaweza kukusababishia madhara makubwa.
Hii inajiri baada ya madaktari mjini Leicester kumtibu mtu mwenye umri wa miaka 34 ambaye alipusuka koo kwa kujaribu kujizuia kupiga chafya.
Huku kukiwa hakuna nafasi ya hewa ya chafya hiyo kutoka, ililazimika kupasua tishu laini.
Licha ya kwamba kisa hicho sio cha kawaida, madaktari wameonya kwamba watu wengine wanafaa kujua kuhusu hatari hiyo.
Kuzuia kupiga chafya kunaweza kuharibu masikio mbali na kuathiri ubongo wameonya katika jarida la BMJ.

Mtu huyo anasema kuwa alihisi kuwashwa katika koo yake baada ya chafya hiyo na muda mchache baadaye akaanza kuhisi uchungu na akaanza kushindwa kula na kuzungumza.

Wakati madaktari walipomchunguza waligundua kwamba alikuwa ana uvimbe katika koo na shingo yake.
Picha za X ray zilizopigwa zilibaini kwamba kuna hewa inayotoka kupitia tushu laini zilizopasuka kupitia shingo yake.
Mtu huyo alilazimika kulishwa kwa kutumia paipu kwa siku saba mfululilizo ili kutoa fursa kwa tishu hizo kupona.
Baada ya kulazwa hospitalini kwa juma moja, mtu huyo alienda nyumbani ambapo alipona.

No comments:

Post a Comment