Katika kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha mapinduzi CCM, na kuunga mkono juhudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyejipambanua kuwasimamia na kuwatetea watanzania wanyonge,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John L. Kayombo Aliyesimama
Moja ya Madarasa yaliyopokelewa leo ambayo yametengenezwa pamoja na madawati na miundombinu muhimu ya kusomea wanafunzi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mheshimiwa John Lipesi Kayombo, sambamba na mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Kisare leo wamepokea madarasa mawili yaliyojengwa na wadau wa maendeleo wanaifanya shughuli zao katika manispaa hiyo ya ubungo madarasa yaliyojengwa katika shule ya Sekondari Urafiki iliyopo kata ya Ubungo
madarasa hayo mawili yaliyojengwa kwa ustadi wa aina yake yamejengwa baada ya kukubaliwa kwa maombi ya Mkurugenzi huyo kwa kampuni ya Tanzania Steel Pipes LTD ya jijini hapa na kwamba sehemu kubwa ya madarasa hayo yamejengwa kwa chuma
‘’wakati
nateuliwa kuwa mkurugenzi nilifanya ziara kwenye shule hii nilikuta hapa kuna
madarasa matano yamechakaa kabisa hayapaswi kutumiwa na wanafunzi wetu,
niliagiza mara moja yavunjwe na tutafute pesa kwa ajili ya kujenga madarasa
mengine matano mapya…kwa neema ya Mwenyezi Mungu tulikutana na hawa watu wa
viwanda tukazungumza nao nikawaomba watujengee madarasa mawili’’. Alisema Mkurugenzi
Kayombo wakati akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Ubungo kutoa hotuba ya kuopokea madarasa
hayo
‘’niseme tu
mheshimiwa mkuu wa wilaya, tutayatunza madarasa haya, ni madarasa ya mfano
hayapo wilaya ya ubungo na mkoa wa Dar es salaam hayapo, hapo hapa Urafiki
Sekondari’’. Alipngeza Kayombo
taarifa zaidi kuhusu madarasa hayo tutawaletea.
No comments:
Post a Comment