WADHAMINI WETU
Friday, December 2, 2016
DANIEL ZENDA AZIDI KUTAKATA: MAKATIBU 32 SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, WAPIGWA SEMINA KUWAJENGEA UWEZO
Shirikisho
la Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, limefanya semina ya utendaji kwa makatibu wake wote wa matawi katika mkoa wa Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kazi zao ili kuliimarisha Shirikisho na Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda alisema, katika semina hiyo iliyofanyia Novemba 30, mwaka huu, jumla ya Makatibu 32 walihudhuria na kuondoka wakiwa wameongeza upeo wao katika kazi zao za chama.
Alisema, moja ya mambo ambayo walifundwa Makatibu hao ni namna nzuri ya kuwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata wanachama wapya miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu, kwa kuwa tegemeo na uhai wa Shirikisho hilo ni wanafunzi wa aina hiyo.
"Unajua Shirikisho linatilia mkazo sana katika kuhakikisha Makatibu wa Matawi wanashughulika kwa juhudi kubwa kuhakikisha kila wakati tunapata wanachama wapya hasa hawa wanaokuwa wanajiunga katika vyuo katika mwaka wa kwanza kwa kuwa hawa wanakuwa bado wabichi na wenye nguvu kutumikia Shirikisho na Chama kwa jumla", alisema Zenda na kuongeza.
"Shirikisho linalipa kipaumbele suala la kuingiza wanachama kutoka wale wa mwaka wa kwanza kwa sababu kuingia kwa wanavyuo wapya vyuoni kuna kuwa na maana pia kuwa wapo wanaondoka kutokana na kuhitimu masomo yao, ambao baada ya kuhitimu wanaweze kushindwa kuendelea kuwa wanachama wazuri wa shirikisho kutokana na kubanwa na shughuli nyingine".

Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda akiongoza semina hiyo
🔺Washiriki
wakiwa kwenye semina hiyo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya
Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar es Salaam
WAZIRI MAKAMBA ALIPOKUTANA WAHARIRI KUZUNGUMZIA ZIARA YA MAZINGIRA KATIKA MIKOA KUMI NCHIN
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akionyesha kwa Wahariri wa vyombo vya habari, picha tofauti za maeneo mbalimbali aliyotembelea wakati wa ziara yake ya kutembelea Mikoa 10 Nchini kuangalia athari za mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi akiongea wakati wa Mkutano huo.
Sehemu ya Wahariri na Waaandishi wa Habari mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba alipoongea nao Ofisini kwakae kuongelea ziara yake aliyoifanya kwa mikoa 10 Nchini.
RC MAKALLA NA OPERESHENI WEKA JIJI SAFI NA ONDOA MSONGAMANO MBEYA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiwa ameongozana na baadhi
ya waendesha Bajaj wa eneo la Kabwe Jijini Mbeya, wakati alipofika
kukutana nao ili kuwasikiliza, ambapo amesitisha kwa muda kuhamishwa kwa
Waendesha Bajaj hao kituoni hapo mpaka hapo kituo kilichopendekezwa wao
kwenda kifanyiwe marekebisho, pia ameagiza kuendelea kwa operesheni kwa
Bajaji kufuata ruti na vituo walivyopangiwa ili kuepusha misongamano
isiyo na lazima na kuhakikisha usafi unaendelea ili jiji la Mbeya liwe
mfano wa kuigwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na vijana hao wanaojishughulisha na Uendeshaji wa Bajaj za abiria, eneo la Kabwe, Jijini Mbeya.
Baadhi
ya madereva wa bajaji watumiao eneo la kabwe kuegesha bajaji zao
wakizungumza na mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla (hayupo pichani). Na Mr.Pengo MMG-Mbeya.
TANAPA KUPANDISHA WATU MLIMA KILIMANJARO KUADHIMISHA SHEREHE ZA UHURU
meneja Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi wa kwanza kushoto Habari Picha na Woinde Shizza,Arusha
Aliyekuwa mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa jenerali msataafu geogre waitara anatarajiwa kuongoza msafara wa zoezi la kupanda mlima kilimanjaro desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa tanzania,
Aidha katika msafara huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka jeshi la wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha jamii kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema kuwa mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia hilo imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii (ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
Alisema kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi mashuhuri wa jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili kuhamasisha watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo litajulikana kama Uhuru Epedition .
Kijazi alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea vufutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka nje ya nchi.
"Katika maadhimisho haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze kupanda mlima kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani tunavyo vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue wanazo fursa "aliongeza kijazi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani wengi wao wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Tours Zainabu Anselm akiongea juu ya kampuni yake ambapo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio vilivyopo ndani ya nchi yetu na sio kuendelea kuviona kwa mbali tu na kuvisikia
kampeni ya Mti wangu yapamba moyoAirtel yaungana na Rc Makonda.
Ongezeko la shughuli za kibindamu na viwanda kwa ujumla
imesababisha kuongezeka kwa hewa ya ukaa na majanga yatokanayo na
mabadiliko ya tabia nchi mfano mafuriko na joto kali ambalo husababisha
magonjwa na athari kwa viumbe hai na binadamu kwa ujumla hasa katika
miji mikubwa ikiwemo jiji la Dar es salaam.
Katika kutekeleza na kuunga mkono kampeni ya utunzaji wa mazingira maarufu kama “mti wangu” iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es saalam , Mh Paul Makonda, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na wafanyakazi wake leo imeshiriki katika kupanda majani , miti na kuweka mbolea ili kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya kuvutia
Bustani hiyo inayoanzia katika mataa ya Moroco hadi maeneo ya mgahawa wa Best Bite katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi ilikabidhiwa kwa kampuni ya Airtel na mh. Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kuboresha na kutunza mazingira ya jiji la Dar es saalam
Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hii, leo wafanyakazi wa Airtel kwa kushirikiana na serikali tunashirikia katika zoezi la kupanda majani na miti katika eneo la katikati ya barabara. Airtel tunaamini ili tuweze kufanya biashara tunahitaji mazingira bora na kwa kupitia kampeni hii ya mti wangu tunaunga mkono juhudi hizo kwa kuyatunza mazingira yanayotuzunguka na kuyaweka katika hali ya usafi na kuvutia” alisema Airtel Afisa Mazinga wa Airtel ,Bwana Ncheye Mazoya
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa wilaya ya Kinondoni, Bwn Awadhi Kinajambo alisema “tunatoa shukurani kwa kampuni ya Airtel kwa kuunga mkono jitihada hizi za kutunza mazingira kupitia kampeni hii mahususi ya “Mti Wangu”. Tunaanmini juhudi hizi zitasaidia katika kuboresha hali hewa,kuondoa tishio la majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupendezsha jiji letu la Dar es salaam”.
Natoa wito kwa wakazi na wafanyabiashara wa maeneo haya kutokatiza kwenye bustani hii wala kutupa taka ili tuweze kuunga mkono kwa vitengo zoezi hili kuwa la mafanikio na kwa pamoja kutunza mazingara yetu.

Afisa Mazingira wa Airtel, Ncheye Mazoya akimwagilia mti baada ya kuupanda, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliposhiriki kupanda majani, miti na kuweka mbolea katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda. Kushoto ni Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Awadh Jambo.

Wafanyakazi wa Airtel wakishiriki kupanda miti katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

Wafanyakazi wa Airtel wakishiriki kupanda majani katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

HABARI MBAYA : WILAYA YA KAKONKO KIGOMA HATARINI KUPOROMOKA KIUCHUMI
WILAYA
ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imeelezwa kuendelea kuporomoka kiuchumi kutokana na mzunguko mdogo wa fursa za kibiashara kupelekwa wilaya ya jiran na watumishi wa idara inayohudumia wakimbizi katika kambi ya mtendeli kuishi Wilayani Kibondo, hali inayo pelekea shughuli zao zote kufanyika Wilayani humo.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagala alitoa wito kwa watumishi hao kutoa fursa za kiuchumi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kakonko wakati wa ujenzi wa nyumba za kudumu za wakimbizi, lengo likiwa ni kuongeza mzunguko wa kibiashara
kwa Wananchi wanao izunguka kambi hiyo na kuacha tabia ya kutoa tenda zote za ujenzi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kibondo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani humo, Ndagala alisema watumishi
wengi wa Kambi ya mtendeli wamekuwa wakifanya biashara na wafanya biashara wa Kibondo,wakati kambi hiyo inahudumia wakimbizi katika Wilaya ya Kakonko hali inayo pelekea uchumi wa wananchi wa Kakonko waliotegemea kuupata kupitia kambi hiyo kuanzishwa kukosekana na kuhamia wilya nyingine ya Kibondo.
Ndagala alisema halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ni halmashauri ambayo uchumi wake bado upo chini,unahitaji kuinuliwa hivyo akawaomba wafanyakazi wa kambi ya Mtendeli pamoja na
shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoa vipaumbele kwa Wananchi wa Wilaya ya Kakonko ili kuinua uchumi wa Wilaya hiyo kwa kuwapatia ajira za ujenzi na ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa wafanya biashara wa Kakonko.
Hata hivyo Mkuu huyo aliwaomba watumishi wote wa Kambi hiyo na mashirika yanayo hudumka wakimbizi kurudi kuishi Kakonko kwakuwa sababu iliyo kuwa ikiwapelekea waishi Kibondo ya kukosekana kwa Nyumba za kupanga Wilayani humo limekwisha Wananchi wamejitahidi kujenga nyumba zenue ubora ambazo wanaweza kupanga na kufanya kazi zao za kuhudumia wakimbizi wakiwa wilayani humo.

Subscribe to:
Posts (Atom)