meneja Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi wa kwanza kushoto
Habari Picha na Woinde Shizza,Arusha
Aliyekuwa
mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa jenerali msataafu
geogre waitara anatarajiwa kuongoza msafara wa zoezi la kupanda mlima
kilimanjaro desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
55 ya uhuru wa tanzania,
Aidha katika msafara huo
wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka jeshi la
wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha
jamii kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na
vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema kuwa
mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia hilo
imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii
(ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha
watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
Alisema
kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi
mashuhuri wa jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili
kuhamasisha watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo
litajulikana kama Uhuru Epedition .
Kijazi
alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni
mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa
mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea
vufutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka
nje ya nchi.
"Katika maadhimisho haya tuna malengo
ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze kupanda mlima kilimanajaro
pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani tunavyo vivutio 16 ambavyo
vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote wanufaike navyo
sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue wanazo fursa
"aliongeza kijazi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania wanapaswa kujitokeza kwa
wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani wengi wao wamekuwa na
mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na kutembelea
hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali inayowafanya
watanzania kupoteza haki yao.
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Zara Tours Zainabu Anselm akiongea juu ya kampuni yake
ambapo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio
vilivyopo ndani ya nchi yetu na sio kuendelea kuviona kwa mbali tu na
kuvisikia
No comments:
Post a Comment