WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, December 13, 2016

BREAKING NEWS: SHIBUDA AJITOSA UWENYEKITI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Tokeo la picha la john shibuda
PICHANI: John Shibuda alipokutana na Rais JohnMagufuli hivi karibuni. kulia ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa UDP John momose Cheyo..

Taarifa zilizotufikia mchana huu zinasema kuwa Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA mheshimiwa John Magale Shibuda anayetambulika kwa jina la utani Drogba, leo amepitishwa na kamati kuu ya  chama chake kuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Baraza la vyama  vya siasa nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha   APPT MAENDELEO ambacho kimefutwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

alipotafutwa na JAMVILAHABARI shibuda amekiri kuteuliwa na chama chake na kuthibitisha kwamba yupo tayari kugombea nafasi hiyo ili awe kiunganishi bora miongoni mwa vyama vya siasa.
''vyama vya kisiasa vinahitaji sauti yenye maono ya busara na hekima, ya itifaki za utawala bora wa siasa na Demokrasia inayoenda sambamba na mfumo wa mapinduzi ya utumishi wa serikali ya awamu ya tano''. alisema Shibuda.
''vilevile dhamana ya mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa inapashwa kuwa na hazina ya welevu wa ufahamu wa historia ya taifa hili la jamhuri ya muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanzania bara na Zanzibar''..

uchaguzi wa mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa unatarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu Desemba 2016 jijini Dar  es salaam ambapo wajumbe wake ni viongozi wawili wawakilishi wa vyama kutoka Tanzania bara na zanzibar na secretariet yake ikiwa chini ya Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inayohesabika kama katibu.
JAMVILAHABARI litaendelea kuwajuza hatua kadha wa kadha kuhusiana na uchaguzi huo muhimu kwa mustakabali wa siasa hapa nchini.

No comments:

Post a Comment