Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza
kutoa heshima zao za mwisho kwa Jayalalithaa Jayaram, mmoja wa wanasiasa
mashuhuri nchini India,.
Mwili wake, ukiwa umevikwa bendera ya India, umewekwa kwa ajali ya kutazamwa na umma katika ukumbi mkubwa katika makao makuu ya jimbo hilo.
Alikuwa anaenziwa sana na wafuasi wake, baadhi ambao walikuwa wanamwita "Amma" (mama) na kuna wasiwasi kwamba huenda baadhi wakaamua kujidhuru au kuzua ghasia.
Awali, baada ya taarifa za kifo chake kutangazwa, kulitokea makabiliano kati ya polisi na wafuasi wake nje ya hospitali hiyo ya kibinafsi ya Apollo. Taarifa hizo baadaye ziliondolewa, ingawa saa chache baadaye alithibitishwa kufariki.
Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakilia hadharani na kujipiga vichwa na vifuani.
Polisi wa ziada wametumwa kudhibiti waombolezaji na kushika doria huku kukiwa na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo.
Jimbo la Tamil Nadu limetangaza siku saba za maombolezi.
Serikali kuu mjini Delhi nayo imetangaza Jumanne kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kama heshima kwake.
Waziri Mkuu Narendra Modi atahudhuria ibada ya mazishi ya kiongozi huyo ambayo yatafanyika baadaye Jumanne.
Jayalalitha aliishi maisha yenye visa vingi, hadharani na faraghani.
Aliigiza katika zaidi ya filamu 100 kabla ya kujiingiza katika siasa.
Jayalalitha baadaye alichukua udhibiti wa chama cha AIADMK kutoka kwa mke wa mwanzilishi wa chama hicho, na kisha akashinda uchaguzi 1991.
Alikuwa ametuhumiwa kwa kujihusisha na ufisadi, na alikaa jela vipindi viwili vifupi, karibuni zaidi 2014.
Mahakama kuu mjini Karnataka ilimuondolea makosa mwaka 2015 na akarejea uongozini.
BBC
No comments:
Post a Comment