Rais Vladmir Putin wa Urusi
Msako
mkali unaendelea kutafuta miili ya askari wa Urusi walio waliokuwemo
kwenye ndege iliyopata ajali kwenye bahari nyeusi iliyoanguka na kuua
askri wote tisni na mbili waliokuwemo .
Wafanyakazi
zaidi ya elfu tatu, wakiwemo wazamiaji zaidi ya elfu moja wako kwenye
harakati za utafutaji manusura ama maiti za askari hao katika eneo la
tukio.
Ndege
iliyokuwa imebeba askari hao ilianguka dakika tatu baada ya kuanza
safari kutoka katika mji wa Sochi ikiwa njiani kuelekea nchini Syria.
Abiria
walio wengi walikuwa ni askari wa Urusi waliokuwa katika shamra shamra
za sherehe za tamasha la kimuziki la Alexandrov wanaojulikana kama kwaya
ya jeshi jekundu.
Ibada ya
kuwaombea marehemu hao imefanyika mjini Sochi na miji mingine tofauti
tofauti kabla ya siku maalumu ya Jumatatu iliyotangazwa kuwa ya
maombolezo.
Mamlaka
nchini Urusi zimetoa tamko kuwa zinafahamu fika wapi ilipo ndege hiyo
katika bahari nyeusi. Mpaka sasa miili saba ya askari imepatikana .Mpaka
sasa hakuna taarifa zozote za kuwepo kwa manusura wa ajali hiyo.
Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini Urusi, Igor Konashenkov, amesema kwamba zoezi la utafutaji linaendelea.BBC
No comments:
Post a Comment