Gazeti lenye Makala ya Rais-Mteule Donald Trump linauzwa katika duka la vitabu nchini Beijing Disemba 12, 2016
China imeeleza siku ya Jumatatu kua imekerwa sana na maoni ya Rais
Mteule wa Marekani Donald Trump akihoji iwapo Marekani iendelee na sera
yake “China moja” kwa sharti kuwa serikali ya China itoe fursa zaidi za
kibiashara.
Katika taarifa ya pamoja kati ya China na Marekani iliyotolewa mwaka
1979, Marekani iliitambua Beijing kama ni serikali pekee halali ya
China, ikikubaliana na msimamo wa Wachina kuwa kuna China moja na Taiwan
ni sehemu ya taifa hilo.Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China amesema kuwa sera
inayokubali Taiwan ni sehemu ya China ndio msingi wa uhusiano kati ya
Marekani na China na kusisitiza serikali ya Trump “kuelewa umuhimu” wa
jambo hili.
Global Times inayodhibitiwa na serikali ilieleza kuwa Trump anaonesha
“Si mzoefu” kwa kufikiria anaweza kutumia sera ya Taiwan kulazimisha
mazungumzo ya kiuchumi “na anahitaji kujifunza jinsi ya kushughulikia
masuala ya mambo ya nje kwa unyenyekevu.”
Gazeti hilo la serikali ya Bejing lilipendekeza kwamba iwapo Trump
ataisaidia Taiwan kupata uhuru wake au kuiuziya silaha “hakutakuwa na
sababu ya China kushirikiana na Washington katika masuala ya Kimataifa”
na itaweza kutoa msaada wa kijeshi na msaada mwengine kwa wapinzani wa
Marekani.
Trump atetea mazungumzo yake ya simu
Katika mahojiano na Televisheni ya Fox News Jumapili, Trump
aliendelea kutetea mazungumzo yake ya simu na Rais wa Taiwan, Tsai
Ing-wen, ambayo ni mawasiliano ya kwanza kati ya kiongozi huyo na Rais
wa Marekani au Rais Mteule wa Marekani tangu mwaka 1979, ambapo Marekani
iliafiki Taiwan ni sehemu ya umoja wa China.
Vile vile alisema hataki China kumuambia nini lakufanya.
;Sijui kwa nini lazima tulazimike kufuata sera ya China moja
isipokuwa labda tukiwa tunataka kufanya makubaliano na China yanayohusu
mambo mengine, ikiwemo biashara,” Trump alisema.
Rais wa Taiwan,Tsai Ing-wen rais mteule wa Marekani Donald Trump na Rais wa China, Xi Jinping.
Rais-Mteule aliikosoa China kuhusu sera zake za sarafu, na kuongeza
nguvu zake za kijeshi katika eneo la South China Sea na kushindwa kwake
kuzuia jirani wake Korea ya Kaskazini kufanya majaribio ya silaha za
nyuklia.
“Sisi tunaumizwa sana na vitendo vya China kushusha thamani ya
sarafu yake ikiwa ni pamoja na kuweka ushuru mkubwa katika mipaka wakati
sisi hatuwatozi wao ushuru, na pia kujenga himaya kubwa katikati ya
eneo la South China Sea, jambo ambalo hawatakiwi kulifanya, na
hawatusaidii kabisa na suala la Korea ya Kaskazini,” Trump alisema.
“Unayo Korea ya Kaskazini. Kuna silaha za nyuklia na China haikuweza kutatua hili tatizo na hawatusaidii kabisa.”
Kauli ya Trump inalenga ushuru wa China na Marekani katika bidhaa
zinazouzwa baina yao. China imeweka ushuru wa kati ya asilimia 5 na 9.7
kwa bidhaa za Marekani na Marekani inakusanya asilimia 2.5 na 2.9 ya
ushuru.
Trump alisema ingekuwa sio heshima kutokujibu simu ya kiongozi wa
Taiwan aliyekuwa anampongeza kwa ushindi wake, akiongeza kuwa alikuwa
anaiona number inapiga kwa saa kadhaa na sio kwa wiki au muda mrefu kama
vile baadhi ya taarifa za vyombo vya habari vya Marekani zilivyosema.
“Ilikuwa ni mazungumzo mafupi mazuri sana,” alisema Trump. “Na ni
kwa nini mataifa mengine yavalie njuga na kusema siwezi kuzungumza na
kiongozi huyo.?”
Lakini China imemkosoa Trump kwa hatua ya kupokea simu, lakini
walikuwa hawana maelezo ya papo kwa papo kwa kauli yake alioitoa katika
mahojiano. Baada ya Trump kuongea na Kiongozi wa Taiwan, Wasemaji wa
ngazi za juu wa White House waliwahakishia maafisa wa China kwamba sera
ya Marekani ya “China moja” itabakia palepale.
Sihitaji kupashwa taarifa za ujasusi kila siku
Wakati wa Mahojiano, Trump pia alisema hahitaji kupokea taarifa fupi
za kintelijensia kila siku akidai kuwa ni zenye kujirudia rudia.
Unajua mimi niko makini, Trump alisema. Sina haja ya kuambiwa kitu
kile kile katika maneno yale yale siku baada ya siku kwa miaka 8 ijayo.
Inaweza ikawa miaka minane, na sihitaji hilo kwa miaka minane. Lakini
ninachosema,”Iwapo kitu kitabadilika tufahamisheni.”
Alisema atapochukua urais rasmi Januari 20, watoto wake wakubwa na
viongozi wa kampuni ya Trump wataendesha shughuli za biashara yake
duniani na hatojihusisha na uongozi wa biashara hiyo.
Lakini hakusema jinsi atavyokaa mbali na biashara hizo kwani watu wa
maadili wanashinikiza afanye hivyo ilikuepuka utata wa maslahi binafsi
kwa maamuzi anayoyafanya kama kiongozi wa Marekani.
Trump amepanga kutoa tamko rasmi siku ya Alhamisi juu ya taarifa
kamili ya namna atavyo jitenganisha kutoka katika Taasisi ya Trump atapo
chukua madaraka.
Amesema kuwa yeye “ni mwazi” katika masuala ya mazingira na iwapo
Marekani iendelee kuwafiki makubaliano ya dunia nzima yaliyofikiwa Paris
katika kudhibiti gesi za sumu zinazo zalishwa na greenhouse ambazo
wanasayansi wamekubaliana yanapelekea katika mabadiliko ya hali ya hewa
hatarishi duniani.
VOA
No comments:
Post a Comment