Rais Barack amezungumzia sera dhidi
ya ugaidi na kila kinachopaswa kufanyika katika siku za usoni katika
vita dhidi ya ugaidi bila kuingiza masuala ya ubaguzi.
Akizungumza katika kambi ya jeshi la anga ya MacDill ,Tampa, jimboni Florida,Rais Obama amesema kuwa vita dhidi ya ugaidi,haipaswi kupoteza mwelekeo wake na misingi iliyowekwa.
Obama amesisitiza kuwa Marekani si mahala ambapo raia anapaswa kutembea na kitambulisho mkononi kujihakikisha kuwa si adui. Sisi ni nchi ambayo ilitoa damu,ikafanya jitihada kubwa na kujitoa kuhakikisha tunatokomeza ubaguzi na sheria kandamizi Marekani na Duniani kwa ujumla.
"Sisi ni taifa linalo amini uhuru wa mtu si jambo linaloweza kuchukuliwa kwa dhana ya jumla jumla tu,na kila mmoja wetu anawajibu kuzingatia hilo.Haki ya uhuru wa kusema,kuishi katika jamii iliyo huru na yenye uwazi,na inayoweza kumpinga hata rais.Nchi ambayo unatazamwa kutokana na tabia zako badala ya vile unavyo onekana,jinsi unavyo abudu, ama jina lako la ukoo ni nani,ama asili ya familia yako,hivi ni baadhi ya vitu vinavyotu tofautisha na watawala wenye uonevu na magaidi".
Amewapongeza wale aliowaita ,walisaidia kuifanya Marekani kuwa mahala salama katika utawala wake.
"Tunapaswa kujivunia maendeleo yaliyofikiwa ndani ya kipindi cha miaka nane.Hakuna zaidi ya hapo.Hakuna kundi lolote la nje la kigaidi lililofanikiwa kupanga na kufanya shambulio ndani ya ardhi yetu".amesema Obama
No comments:
Post a Comment