WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, December 13, 2016

MWIGULU NCHEMBA : MAKOSA BINAFSI YA WATU YASIHUSISHWE NA DINI ZAO

Tokeo la picha la MWIGULU NCHEMBApicha ya maktaba ikimuonyesha waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu nchemba akisalimiana na viongozi wa dini hivi karibuni.

Ujumbe wa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwigulu Nchemba kwa watanzania wote alioutoa jana kwenye sherehe za Maulid Iramba-Singida.

1) Mtu aliyeshika sana imani yake si mdini bali ni mcha Mungu, mtu anayesali sana sii mdini bali ni mcha Mungu,
Mdini ni mtu anayebagua dini ya wenzake, anayedharau dini zingine, anayependelea watu au kuchukia watu kwa misingi ya dini zao, tusiwahukumu watu kwakuwa wameshika sana dini zao au kwa kuwa wanasali sana, wanamcha Mungu.
2) Katika hii Dunia,Siku zote makosa yatafanywa na watu wenye dini au wasio na dini. Sasa jambo baya likitendwa na mtu mwenye jina la kikristo basi jambo hilo lisichukuliwe kuwa ni jambo lililofanywa na dini ya kikristo, jambo baya likifanywa na mtu mwenye jina la kiislam lisichukuliwe kuwa ni jambo la dini ya kiislam, bali liwe jambo la mtu binafsi aliyefanya kosa, na tusaidiane kuwafichua wote wanaochafua taswira kwa kufanya maovu.
Vilevile,Mwigulu nchemba ametoa bati elfu moja(1,000) kwaajili ya kuezeka baadhi ya misikiti iliyokwisha jengwa maeno mbalimbali ya wilaya ya Iramba.Pia ametoa Gari aina ya Noah kwaajili ya shughuli za ofisi ya BAKWATA wilaya ya Iramba.
Asanteni kwa kututendea uisilam, kututendea jambo jema hili.
Mwigulu Nchemba, Waziri MNN
12/12/2016
Iramba-Singida

No comments:

Post a Comment