WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, December 22, 2016

MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ANAOMBA MSAADA KITANDANI


Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Simba Sports iliyokuwa
ikiitwa Senderland ,Athur Mwambeta amewaomba wadau mbalimbali wa mchezo
wa soka nchini na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia kupata
chombo cha usafiri kitakachomtoa sehemu moja mpaka nyingine mara baada ya
kukatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomkabili.



Mwambeta amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na
Globu ya jamii katika hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo amelazwa
katika jengo la Kibasila ward namba 11, ambapo anaendelea na matibabu
mara baada ya kukatwa mguu ijumaa iliyopita.



"Nimeugua maradhi haya pindi tu nilipoacha kucheza mpira hali
iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kwanza mwaka 2015 na mwaka huu ijumaa
iliyopita ndipo nilipokatwa mguu wangu wa pili na kubaki kama hivi
mnavyoniona, kwani siwezi tena kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine
kama ilivyokuwa awali hivyo kwa yoyote anaeweza kunisadia naomba
ajitokeze " amesema Mambeta.



Amesema kuwa anaomba wadau kumchangia kupitia nambari hii 0714435312 ili
aweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kimaisha.



Pia alitoa wito kwa wapenzi na wanachama wa CCM kujitokeza kumsadia
kwani wao ni moja ya watu waliokuwa wahamasishaji wakubwa kupitia TANU
mpaka ilipozaliwa CCM walitumia mpira kama sehemu ya hamasa.


 Wachezaji wa zamani wakiongozwa na Kitwana Manara wakimjulia hali,Athur Mwambeta,ambaye amekatwa miguu yote miwili

No comments:

Post a Comment