Ummy Mwalimu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
SAWA wa
kijinsia unaweza kupimika kwa mifano ya kuwepo kwa fursa sawa
au matokeo sawa. Au kwa kifupi, tunaweza kusema kuwa ni haki,
majukumu na fursa sawa kwa wanawake na wanaume.
Ukatili
wa kijinsia ni tatizo ambalo linawanyima uhuru wanaume, wanawake na
watoto kufurahia haki zao za msingi ambazo pia ni haki za binadamu.
Utafiti
uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa mwanamke
mmoja katika kila wanawake watatu katika maisha yake amewahi kufanyiwa
ukatili wa kijinsia ama kimwili, kingono na kisaikolojia.
Ukatili
wa kijinsia umegawanyika katika makundi mbalimbali ikiwemo ukatili wa
kimwili, ukatili wa kisaikolojia, ukatili wa kingono, ukatili utokanao
na mila na desturi, ukatili wa kiuchumi, na ukatili wa kijinsia
sehemu za kazi.
Zipo
sababu mbalimbali zinazopelekea ukatili wa kijinsia ikiwemo, mifumo ya
jamii isiyozingatia usawa baina ya wanawake na wanaume, wanawake
kutokuwa na sauti na ushiriki kwenye vyombo vya maamuzi ndani ya jamii
na mitazamo hasi ya wanajamii kwa wanawake, pamoja na mfumo dume kwenye
jamii.
Sababu
nyingine ni umasikini, kuanguka kwa mifumo ya kijamii inayolinda maslahi
ya wanajamii, ukimya wa jamii kukemea matendo ya ukatili wa kijinsia,
na kukosekana kwa utekelezaji wa sheria za kudhibiti vitendo vya ukatili
wa kijinsia.
Hvi
karibuni Serikali ilizindua Mpango Kazi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya
Wanawake na Watoto (2017-22) unaolenga kushirikisha wadau mbalimbali
kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na hivyo kusaidia wahanga wa
ukatili huo kupata huduma stahiki ili kudhibiti ukatili nchini
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema
kuwa jamii ina jukumu kubwa la kuhakikisha ukatili wa wanawake na
watoto unapigwa vita kwa vitendo
“Serikali
inaikumbusha jamii kupambana na vitendo vya ukatili kwani ukatili
unafanyika kuanzia ngazi ya familia hivyo ni jukumu la wananchi kutoa
taarifa za ukatili wa wanawake na watoto ili vyombo vya dola viweze
kuchukua hatua za kisheria”, alisema Waziri Ummy
Aidha
Waziri Ummy aliongeza kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya ukatili
yanayosababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umaskini katika
familia, mila na desturi potofu zenye athari katika jamii, malezi na
makuzi mabovu na sheria kandamizi.
Naye
Mwakilishi wa Asasi za Kiraia zinazoshughulika na utetezi wa haki za
watoto (TCRF), Erick Guga alisema watoto ndiyo wahanga wakubwa wa
ukatili huo hivyo ni wakati mwafaka kwa mpango kazi kuanza kazi ili
kuwanusuru wanawake na watoto katika ukatili
“Mpango
Kazi huu wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini
Tanzania utakuwa ndiyo dira kwa wadau wote wa masuala ya maendeleo ya
wanawake na watoto hapa nchini hivyo ni vema Serikali kushirikiana na
wadau kila inapohitajika”, alisema Bw. Guga.
Waziri wa
Fedha na Mipango Philip Mpango alizitaka Wizara, Taasisi zote za
Serikali, Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanazingatia Mpango huo kwa
kutenga fedha katika bajeti zao ili kukidhi utekelezaji wa shughuli
zilizopangwa.
“Hata
hivyo nazitaka taasisi zote zilizo chini ya Wizara yangu kutokomeza
ukaliti wa wanawake mahali pa kazi na nitawachukulia hatua wale
watakaojihusisha na ukatili huo” alisema Waziri Mpango.
Alisema
kuwa athari ya madhara ya kuendelea kwa ukatili dhidi ya wanawake na
watoto ni kubwa kijamii na kiuchumi ambapo kwa mujibu wa takwimu za
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 asilimia 51.3 ya wanawake nchini,
watoto chini ya miaka 18 ya watanzania walifanyiwa ukatili.
Kwa
upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi,
vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, alisema kuwa ofisi
yake itatoa miongozo ya kisheria katika utekelezaji wa mpango huo.
Alisema
kuwa suala la kutokomeza ukatili si la Serikali pekee bali kuwataka
Sekta binafsi, asasi za kirai na wadau wa maendeleo kuungana
Waziri wa
Mambo ya Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema kuwa katika
Wizara yake inaandaa mkakati wa kushirikisha wananchi kutoa maoni kuhusu
sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kufanya mapitio ya pitia sheria ya mtoto
ili kuweza kutokomeza suala la ukatili katika jamii.
Naye
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Sihaba Nkinga alisema kuwa, kabla ya kuandaliwa kwa Mpango Kazi huu,
Tanzania ilikuwa na mipango kazi minane (8) ya kuzuia ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
Akifafanua
zaidi Sihaba alisema kuwa mipango hiyo haikuwa na mfumo wa kutokana na
madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maendeleo ya nchi,
wakuu wa nchi wanachama wa Umoa wa Mataifa waliazimia kwa pamoja
kutokomeza ukatili huo kupitia utekelezaji wa lengo Na. 5 na 6 ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030.
“Tanzania
ni kati ya nchi nne (4) za kwanza duniani na nchi pekee katika Afrika
iliyowezeshwa kupitia jukumu lilioanzishwa la kusaidia nchi wanachama wa
Umoja wa Mataifa kuandaa mpango wa kuzuia na kuitikia afua za kudhibiti
ukatili”, alisema Sihaba.
Mpango
huo unatarajiwa kuwezesha na kuondoa ukatili dhidi ya wanawake kwa
asilimia 50 kufikia mwaka 2021/2022; na kuondoa ukatili dhidi ya watoto
kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2021/2022, na hivyo kuleta mabadiliko
makubwa kwa kuwa na familia salama, na jamii yenye utulivu.
Kazi
zitakazotekelezwa na kila mdau kuanzia familia, jamii, halmashauri,
mikoa, wizara, sekta binafsi, asasi za Kiraia na wabia wa maendeleo
Mpango umeweka mfumo fungamanishi wa uratibu, ufuatiliaji na tathmini
ambao utaratibiwa katika ngazi ya Taifa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ngazi
ya mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, na ngazi ya halmashauri na
Wakurugenzi Watendaj
No comments:
Post a Comment