Kiongozi wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe (kulia) akizungumza jambo na Shemeji wa marehemu Mpoki Bukuku, Edwin Mjwahuzi alipokwenda kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani.
Mhariri
Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda akimfariji mjane wa
marehemu Mpoki Bukuku, Lilian nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani, Dar
es Salaam. Bukuku alifariki juzi baada ya kugongwa na gari Barabara ya
Bagamoyo karibu na Kituo cha ITV, Mwenge. PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kibanda akimfariji mama mzazi wa marehemu Mpoki Bukuku
Zitto Kabwe (kulia) akizungumza na kaka wa Marehemu Mpoki, Gwamaka Bukuku wakati wa msiba huo
Waandishi
wa habari wakiwa kwenye msiba wa marehemu Mpoki Bukuku ambaye alikuwa
Mpigapicha mwandamizi wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian
Wanahabari wakijadiliana mambo wakati wa msiba huo
Mmmiliki wa Blogu ya KAMANDA WA MATUKIO BLOG, Kamanda Richard Mwaikenda, ambaye pia ni Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo, Kamanda Richard Mwaikenda (kulia) akiwa na wanahabari wenzie kwenye msiba huo.Kutoka kushoto ni Mpigapicha wa Waziri Mkuu, Hilary Bujiku, Mmiliki wa Blog ya K-VIS, Khalfan Said, Mmiliki wa Blog ya Michuzi, ambaye pia ni Mpiga Piacha na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Muhidini Issa Michuzi, Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Mwananchi, ambaye ni shemeji wa marehemu Mpoki, Edwin Mjwahuzi na Francis Chirwa ambaye ni mmoja wa viongozi wa Bodi ya Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema
No comments:
Post a Comment