MWIGULU NCHEMBA AWAJIBISHWE.
Na Mwl Razaq Mtele Malilo
Kwa kauli ile ya Mwigulu Mchemba, Waziri wa mambo ya ndani juu ya miili ya watu saba iliyokutwa ikielea mto Ruvu inatosha yeye mwenyewe ajiuzulu au Rais achukue hatua za kumwajibisha na Rais akishindwa basi bunge lichukue hatua kwa kuiwajibisha serikali kwa kumtaka Rais amwajibishe waziri huyo au bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Kama sehemu pekee ambayo bunge linaweza kuiwajibisha serikali ikiwa tu yeye waziri husika atashindwa kujiwajibisha na Rais akashindwa kumchukulia hatua waziri huyu.
Na hapa nimkumbushe Rais kuwa kauli ya Waziri huyu juu ya hili ni zaidi ya Kosa la Kitwanga kujibu swali akiwa amelewa pale bungeni.
Wahamiaji haramu zipo sheria za kuwachukulia sio kuwaua na hii ni
uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu haitofautiani na kile walichokuwa
wakikifanya Afrika ya Kusini kuwaua raia wa kigeni eti wananyima fursa.
Hii kauli ya Waziri ina maanisha ni kauli ya serikali na inaweza kuhatarisha mahusiano ya taifa letu dhidi ya mataifa mengine.
Naamini wapo watanzania wengi sana wapo nchi za mbali wanaishi bila kufuata utaratibu kwa maana ni wahamiaji haramu, je Tanzania itafurahia raia wake wauawe huko waliko?
Lakini pia Mchemba ana uthibitisho gani kuwa miili hiyo ilikuwa ni ya wahamiaji haramu? Hii ni kauli ya kukurupuka.
Ndugu zetu iwe Watanzania au si Watanzania inasikitisha kuona hayo yametokea alafu anatokea mtu tena waziri anapayuka mambo ya ajabu...! Huo ndio utawala wa kisheria?
Suala hili si dogo na haitakiwi kulifumbia macho.
Thamani ya binadamu mmoja ni zaidi ya Faru wote duniani, ni zaidi ya tembo wote, ni zaidi ya nyati wote na ni zaidi ya simba wote na zaidi na zaidi.
Inasikitisha ni jambo la kutisha kwa Waziri ambaye alithubutu kuwania nafasi ya Urais kwenye chama chake na Leo kawa waziri lakini amekuwa na kauli za kutisha zaidi ya viongozi wa vikundi vya kigaidi duniani na hii inanipa shaka je mtu Kama huyu angekuwa Rais angelilifikisha wapi taifa letu...
Kauli ya Waziri huyu inaiweka serikali ya nchi yetu mahali pabaya pengine hata watu kuanza kuisi ushiriki wa serikali kuhusu maiti zile na hivyo kutomwajibisha ni kuthibisha hisi za watu hasa wakihusisha hatua za kulega zilizochukuliwa na serikali na hii kauli inaiweka pabaya serikali na nchi yetu na kila mmoja hana budi kuilaani kauli chafu iliyotolewa na Waziri huyu.
NCHEMBA AACHIE NGAZI.
Mtele Malilo The Teacher

No comments:
Post a Comment