Antonio Guterres kutoka Ureno ameapishwa Jumatatu kuwa katibu mkuu wa 9 wa Umoja wa Mataifa.
Antonio Guterres kutoka Ureno ameapishwa Jumatatu kuwa katibu mkuu wa
9 wa Umoja wa Mataifa. Wakati akihutubia mataifa wanachama, Guterres
alisema Umoja wa Mataifa lazima uwe wenye kutekeleza majukumu yake kwa
wakati. Amesema Umoja huo lazima pia uangazie maswala yanayohusu watu
kabla ya kuzingatia zaidi mikakati.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 67 na aliewahi kuwa waziri mkuu 1995- 2002 na pia kiongozi wa shirika la kushughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 2005- 2015, alishinda wagombea wenzake zaidi ya darzeni moja kwenye mchujo wa uchaguzi uliochukua miezi 10.
Gueterres anakabiliana na kibarua kigumu wakati ulimwengu ukishuhudia tatizo la uhamiaji, mapigano kwenye mashariki ya kati na Afrika, ugaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, pindi atakapochukua usukani Januari mosi kutoka kwa katibu mkuu wa Umoja huo anaeondoka Ban Ki –moon.
VOA

No comments:
Post a Comment