waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelea ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi.
waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi, hivi karibuni ameonyesha kukonga nyoyo za watanzania masikini na wanyonge kwa kuwatolea uvivu watendaji wavivu wanaoifanya ofisi na wizara yake kuonekana wanalalia kazi na kutokutoa hati za watu kwa wakati hata kama wameshazilipia kwa visingizio kuwa makamishna wa kusaini na kupitisha hati hizo za ardhi kutokuwepo ama kuwa wachache.
waziri lukuvi amesema hayo hivi karibuni baada ya kupokea malalamiko kwa njia ya meseji kuwa huko mikoani na wilayani, wapo wananchi wamelipia hati na sasa ni miaka mitatu wanafuatilia bila mafaniko yoyote jambo ambalo linaendana tofauti na msimamo na agizo lake alililitoa lakwamba zisizidi siku 30 tangu mtu kulipia na kupewa hati yake ya umiliki wa srfhi.
No comments:
Post a Comment