BOT YAKANUSHA KUTOTUMIKA NOTI YA SHILINGI 500
Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha
wananchi wote kuwa,habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya
kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano haitatumika tena kuanzia
Desemba 31,2016; sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa. Ukweli
ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko
sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka
mikononi mwa wananchi. Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.Marcian Kobello. Mkurugenzi wa Huduma za kibenki- BoT .
No comments:
Post a Comment