Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema
ataonana na Rais mteule wa Marekani Donald Trump mara tu atakapo
apishwa kuingia madarakani.
Putin amewaambia waandishi wa habari kuwa alimuunga mkono Trump ili kuweka sawa uhusiano wa Marekani na nchi yake.
Putin ameongeza kuwa halitakuwa jambo rahisi ukizingatia na namna
nchi zote mbili zinavyotofautiana kimisimamo, lakini atafanya kila
awezalo kuweka mambo sawa zaidi.Juma lililopita, Shirika la upelelezi nchini Marekani CIA liliishutumu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani kwa kumuunga mkono Trump.
BBC
No comments:
Post a Comment