Meneja mwandamizi wa Shughuli za Kibenki DCB Samwel Dyamo akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni
ya boresha maisha na DCB pamoja na Pata faida na DCB itakayoanza kuchezwa kwa droo ya kwanza Desmba 17, Kushoto ni Meneja Masoko Boyd Mwaisame.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI
ya DCB imedhamiria kuendelea kuwa kuwajali wateja wake imeanzisha
kampeni ya "boresha maisha na DCB" na " Pata faida na DCB" itakayoanza
Desemba 17 kwa ajili ya kuwazawadia zawadi mbalimbali pamoja na fedha
taslimu kwa wateja wapya na wa zamni.
Akizungumzia
kampeni hiyo, Meneja mwandamizi wa Shughuli za Kibenki DCB Samwel Dyamo
amesema kampeni boesha maisha na DCB na Pata faida na DCB itadumu kwa
miezi mitatu na kila mwezi kutakuwa na droo moja itakayotoa washindi
watatu wa fedha taslimu laki mbili,
Dyamo
amesema kuwa mbali na fedha taslimu kutakuwa na washindi wengine wawili
watakaopata simu za mkononi na washindi 20 watapata kila mmoja na
watatangazwa mbele ya waandishi wa habari na kukabidhiwa zawadi zao.
Droo
ya kwanza itachezeshwa Desemba 17 na itamalizika Februri 17 na wateja
wanatakiwa kuweka fedha mara kwa mara kwenye akaunti mojawapo ya akiba
binafsi, akaunti ya watoto na akaunti ya WAHI kiasi cha kuanzia sh
50.,000 na kuendelea na kuongeza mana mara mbili zaidi ya sh 500,000.
Dyamo
amesema kuwa, mteja atakayeweka fedha hizo ataingia moja kwa moja
kwenye droo hizo, mbali na kampeni hiyo pia kutakuwa na kutakuwa na Pata
faida na DCB itakayokuwa inawapa faida wateja kwa kuwekeza nkupitia
huduma yetu ya akaunti ya muda mrefu (fixed account) kwa kuweka kiais
cha milioni 50 na kuendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja na watapata
faida ya asilimia 15 ya fedha zako.
Alisisitiza
kuwa, hata kama utaziweka fedha zako kwa kipindi cha miezi sita bado
utaendelea kufaidika zaidi na kuwataka kujitokeza kwa wingi hususani kwa
wajasiramali, watu binafsi na taasisi mbalimbali.
Meneja
wa matawi wa DCB, Haika Machaku amewataka watanzania kujiunga na benki
yao kwani asilimia kubwa ya faida inaenda kwa wananchi kwa ajili ya
miradi mbalimbali.
Meneja wa matawi wa DCB,
Haika Machaku akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa
wananchi kujiunga na benki yao ili kuweza kufaidika zaidi.
No comments:
Post a Comment