Makampuni ya silaha ya Marekani na Ulaya Magharibi yalihodhi katika
biashara ya uuzaji silaha ulimwenguni mwaka 2015, wakati makampuni ya
Urusi na Korea Kusini yakiwa pia yanaongezeka.
Kwa mujibu wa taasisi inayochunguza masuala ya amani duniani yenye
makao yake makuu mjini Stockholm, SIPRI, uuzaji wa vifaa vya kijeshi na
huduma katika nchi 100 za juu duniani zenye silaha, zilikuwa na jumla ya
dola bilion 370.7 ikishuka kidogo kwa asilimia 0.6 ukilinganisha na
mwaka 2014.
Katika makampuni 39 ya kimarekani yaliyoorodheshwa
kati ya makampuni makubwa 100 ya silaha, yanakamata mauzo kwa zaidi ya
nusu ya silaha zilizouzwa ulimwenguni mwaka 2015
Mauzo katika
makampuni ya kimarekani yalikuwa na jumla ya dola bilion 209.7, ikiwa
chini kwa karibu asilimia 3, hali hiyo inaonya kupungua kwa kiwango cha
matumizi nchini Marekani, kupanda kwa thamani ya sarafu ya dola pamoja
na bidhaa nyingine kama vile ndege za kivita.
Kampuni ya
Lockheed Martin imefanya mauzo ya dola bilion 36.4 ikifuatiwa na kampuni
hasimu ya Boeng kwa dola bilion 27.9, na ikifuatiwa pia na kampuni ya
Uingereza BAE sytem kwa dola bilion 25.5
Makampuni yaliyoko Ulaya
Magharibi yalishuhudia kuongezeka kwa mauzo mwaka 2015, na jumla ya
uuzaji ulikuwa ni dola bilion 95.7 ililinganishwa na kushuka
kulikoshuhudiwa mwaka 2014.
Makubaliano ya uuzaji silaha nje ya nchi wachangia ongezeko
Kuongezeka
kwa kiasi kidogo cha asilimia 6.6 cha biashara ya silaha kwa makapuni
ya Ulaya Magharibi kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na makubaliano ya
uuzaji wa silaha nje ya nchi na makampuni ya kifaransa yaliyoko Misri na
Qatar alisema Aude Fleurant kiongozi wa SIPRI anayeshigulika na
mpango wa masuala ya matumizi ya silaha.
Pamoja na kuwa makampuni 10 makubwa ya utengenezaji wa silaha
yanapatikana nchini Marekani au Ulaya Magharibi yanatawala nusu ya mauzo
ya silaha ulimwenguni mwaka 2015, SIPRI inasema kuwa mpango wa muda
mrefu ambao unatazamiwa unaonyesha kuwa kuhodhi kwao kunadhoofika. Mwaka
2012 ushiriki wao ulikuwa karibu asilimia 60.
Makampuni ya Urusi
na Korea Kusini yameongezeka pia katika uuzaji wa silaha, wakati ripoti
hiyo ikikariri kuwa kuna uimara wa uzalishaji nchini India na Uturuki.
Makapuni ya Urusi yanasimamia chini ya asilimia 10 ya mauzo katika
orodha hiyo, kampuni kubwa ya Urusi ilikuwa na mauzo ya dola bilion 6.9,
katika nafasi ya jumla imeshika nafasi ya 13.
Manunuzi ya silaha
ndani ya nchi pamoja na uuzaji wa silaha nje ya nchi umesaidia kuongeza
mauzo ya silaha kwa karibu dola bilion 7.7 ya makampuni 7 ya Korea
Kusini yaliyo katika orodha.
Kutokana na kutokuwepo kwa taarifa
za kutosha makapuni ya China hayakuwekwa katika orodha, japo SIPRI
inakadiria kuwa makapuni 9 ya kichina yangeweza kuingizwa katika orodha
hiyo.
DW
Mwandishi: Celina Mwakabwale/DPA
Mhariri:Yusuf Saumu
No comments:
Post a Comment