PROF. MBARAWA: ANDAENI WATAALAMU WA KUTOSHA
Mkuu wa
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zakaria Mganilwa akitoa
taarifa ya utendaji wa chuo hicho kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Baraza la Chuo
hicho, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
mpya wa Baraza la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Bavon
Nchomba akifafanu jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Baraza la Chuo hicho, jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na
wajumbe wa Baraza la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), katika
uzinduzi wa Baraza jipya la Chuo hicho, jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakisikiliza hotuba ya Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika
uzinduzi wa Baraza jipya la Chuo hicho, jijini Dar es Salaam.
Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimetakiwa kuchangamkia fursa za kuandaa
wataalam wa kada mbalimbali za usafirishaji wa anga ili kuinua sekta
hiyo na kuiwezesha nchi kujulikana Kimataifa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Baraza la Chuo hicho, Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa
kuzalisha wataalam pekee haitoshi bali ni jukumu la uongozi wa Baraza
hilo kuhakikisha wanawasaidia wataalam hao kwa kuwaunganisha na
mashirika makubwa ya usafirishaji lengo ni kuwajengea uwezo na
kuwatambulisha kimataifa.
“Tayarisheni
wataalamu na muwakutanishe na Wakurugenzi wakuu wa Makampuni kama
Emirates, Qatar na Etihad ili kuwawezesha kupata fursa kirahisi na wao
kuweza kuonekana kimataifa”, amesema Profesa Mbarawa.
Ameongeza
kuwa Chuo kinahitaji kuchukua wafanyakazi kutoka Kampuni ya Reli
Tanzania (TRL), ili kutoa mafunzo kwao kwa ajili ya kuzalisha wataalam
wenye ujuzi na uwezo wa kujenga miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa reli
ya kisasa (Standard Guage).
“Msipotumia
fursa kama hizi za kuandaa wataalamu wa mbalimbali, tutakosa watalaamu
wazawa wa miradi mikubwa na kuanza kulalamika kuwa Chuo kipo lakini
hakithaminiki kumbe mwanzoni tulishindwa kujipanga”, amefafanua Waziri
Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amelipongeza baraza lililopita kwa uwezo mkubwa wa kukusanya
mapato ya ndani yatokanayo na ada za wanafunzi kutoka Bil. 2.1 kwa mwaka
wa fedha 2011/2012 hadi kufikia Bil. 5.1 mwaka 2015/2016.
Aidha,
Prof. Mbarawa ameutaka uongozi wa Chuo hicho kuweka mifumo imara ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ili kuweza kuwajengea
mazingira mazuri kati ya Walimu na Wanafunzi.
Sambamba
na hilo, ameutaka uongozi kupunguza idadi ya kozi zinazotolewa chuoni
hapo na kuwa na kozi chache zenye tija na soko kimataifa ili kukifanya
chuo hicho kuwa cha kipekee Afrika.
Kwa
upande wake Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Prof. Bavon Nchomba
amemhakikishia Waziri huyo kushughulikia changamoto zote zinazoikabili
chuo hicho kwa kuanzia na upunguzaji wa idadi za kozi zisizo na tija.
No comments:
Post a Comment