WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Friday, December 30, 2016

MBUNGE CCM AADHIBIWA KUCHOCHEA MIGOGORO

CCM KASULU YATOA ADHABU KWA MBUNGE NA MADIWANI WAKE KWA TUHUMA ZA KUCHOCHEA MGOGORO WA KUMPINGA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU


Na Rhoda Ezekiel- Kigoma,

KAMATI ya usalama na maadili na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kasulu imetoa adhabu kwa Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa kigoma,Josephin Ngezabuke na madiwani sita wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kwa tuhuma za kuchochea mgogoro wa madiwani kumpinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwamba aondolewe hafai.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katibu muenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud Kitowe alisema kumekuwa na mgogoro Mkubwa uliodumu kwa miezi mitano wa Baadhi ya madiwani wa Act na CCM waliomuandikia barua Mkurugenzi ya kudai Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kasulu aondolewe hafai na Chama Cha mapinduzi hakikupatiwa barua hiyo ambayo ingeweza kuwasaidia kujua chanzo cha tatizo nini.

Alisema katika mgogoro huo madiwani wa CCm walio shiriki ni watano na kati ya hao mmoja ambaye ni Seleman diwani wa kata ya Kumnyika amepewa adhabu ya kalipio ambayo ataitumikia kwa miezi 18 kwa kosa na kushiriki kuandika barua ya kumkataa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati jambo hilo bado halijajadiliwa katika Kikao cha Chama kwamujibu sisi kama chama tulipo pata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi tuliwaita madiwani walio husika na kupewa onyo.


Aidha kitowe alisema madiwani wanne waliojiorodhesha kwenye barua ya kushiriki kumpinga Mwenyekiti huyo kamati ya siasa pia imetoa adhabu ambayo kwa Mujibu wa Sheria za Chama cha mapinduzi hairuhusiwi kuitangaza hazarani nao watatumikia adhabu hiyo kwa miezi 12.

Alisema Madiwani hao walipo hojiwa walikili mgogoro huo una chochewa na baadhi ya watu ambao ni Diwani wa Kata ya Murusi Steward Zinduse ambae alikuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiyi wa halmashauri akashindwa pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kigoma Josephini Ngezabuke nao pia wamepewa adhabu ambayo hairuhusiwi kitangazwa kwa mujibu wa sheria na barua walishapewa zinazo elezea adhabu zao.

No comments:

Post a Comment