Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza
kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia leo jioni moshi
inaendelea kutanda. Kilichosababisha moto huo hakikajulikana.
Shughuli
za kuzima moto bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi
vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.
Hilo Ni
gereza linalohifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na wengine
wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni Victoire
Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4 iliyopita Kwa
hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.
Viongozi kadhaa serikalini wamefika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi.
Bado Ni
mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari
hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza kuu ya Kigali.
Magari ya
zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa
wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa.BBC
No comments:
Post a Comment