Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye kofia)
akiambatana na timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya
Mipango, watumishi wa Bandari ndogo ya Kilwa pamoja na maofisa kutoka
Halmashauri ya Kilwa wakielekea ukaguzi wa maeneo mbalimbali katika
Bandari ya Kilwa Masoko.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiulizia juu
ya utendaji kazi wa kivuko (hakipo pichani) wakati wa ziara ya Tume ya
Mipango katika Bandari ndogo ya ya Kilwa masoko.
Kivuko
kilichopo katika Bandari ya Kilwa Masoko ambacho hakitumiki mara kwa
mara ambapo wanachi hutumia boti zinazotoza nauli ya shilingi 1,000.
Afisa
wa Bandari ndogo ya Kilwa Masoko, Bw. Abubakar Bashir akimuonesha Kaimu
Katibu Mtendaji sehemu iliyotengwa (haipo pichani) kwa ajili ya
shughuli za uvuvi ili kuepusha muingiliano wa shughuli za bandari na
shughuli zingine. Wengine ni Bw. Senya Tuni (kulia) na Bw. Andrew
Aloyce, wachumi kutoka Tume ya Mipango.
Shughuli za uvuvi na usafiri wa boti zikiwa zimetengewa sehemu maalaum ili kuepusha mwingiliano na shughuli za Bandari.
Barabara inayoingia kwenye gati ya Bandari ndogo ya Kilwa Masoko.
Mhandisi
Omari Athuman (mwenye shati ya Mikono mirefu) akimuonesha jambo Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri juu ya Bandari ndogo
ya Kilwa Masoko.
Na Adili Mhina, Kilwa.
Mamlaka
ya Bandari imeshauriwa kuiangalia bandari ndogo ya Kilwa Masoko katika
kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili kuongeza ufanisi wa shughuli
bandari hapo ikiwa ni njia mojawapo ya kuweka mazingira mazuri kwa
wafanyabiashara nchini.
Ushauri
huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya
Mipango Bibi Florence Mwanri alipoiongoza timu ya wataalamu wa ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango kukagua shughuli za
maendeleo katika bandari hiyo.
Katika
ziara hiyo, Mwanri alionesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa bandari
hiyo baada ya kubaini kuwa hakuna tishari wala vifaa vinavyoweza
kutumika katika kupakia na kupakua mizigo huku akielezwa kuwa
mfanyabiashara anapoleta meli banadarini hapo analazimika kutafuta vifaa
vya kupakulia mizigo yake mwenyewe.
“Bandari
hii ni fursa kubwa kiuchumi haipaswi kuwa katika hii wakati Serikali ya
sasa inajitahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara. Hivyo, ni
muhimu kwa Mamlaka ya Bandari kupitia bajeti yao kuangalia uwezekano
wa kupata vifaa hivyo ili kuondoa usumbufu na gharama kwa
wafanyabiashara wanaotumia bandari hii,” alisema.
Alieleza
kuwa kwa sasa bandari hiyo inaweza kufanya vizuri na kuwa na uwezo wa
kujiendesha yenyewe kama mazingira yake yataboreshwa kwa kuwa shughuli
za usafirishaji zinaweza kuchangamka baada ya kiwanda cha saruji
kujengwa eneo hilo huku kiwanda cha mbolea na kiwanda cha kuchakata
mihogo vikitarajiwa kujengwa Kilwa.
Alieleza
kuwa uwekezaji katika eneo hilo ni muhimu kwani bandari hiyo pia
inatumika kusafirisha watalii kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na
kuwepo vivutio mbalimbali vya utalii katika Wilaya ya Kilwa.
Hata
hivyo, Mwanri alisisitiza kuwa kabla ya kufanya uwekezaji mkubwa
bandarini hapo ni lazima ufanyike upembuzi yakinifu ili kuwa na taarifa
za kisayansi juu ya aina ya uwekezaji unaohitajika. Utafiti wa soko pia
unahitajika kuweza kubaini fursa za kibiashara zinazoweza kupatikana
ikiwa uwekezaji mkubwa utafanyika.
Bandari
ya Kilwa Masoko inaelezwa kuwa ipo katika mazingira mazuri kijiografia
kwa kuwa eneo hilo la bahari halina upepo mkali unaoweza kuleta usumbufu
wakati meli zinapotia nanga. Vile vile bandari hiyo ipo karibu na Dar
es Salaam hivyo inaweza kutumika kusapunguza mlundikano wa mizigo katika
Bandari ya Dar es Salaam.
Tofauti
na bandari zingine, Bandari ya Kilwa Masoko inaelezwa kuwa na kina
kirefu zaidi ambapo katika lango la lake kuna kina cha takribani mita 60
hivyo meli kubwa zinaweza kufika bandarini hapo bila kuingia gharama
za uchibaji kwa ajili ya kuongeza kina.
No comments:
Post a Comment