Wakili Thomas Msasa.
Nyota ya wakili msomi maarufu mjini kigoma na Tanzania kwa ujumla Thomas Msasa imezidi kung'aa ambapo tunaelezwa kuwa amezidi kushinda kesi mbalimbali alizokuwa anazisimamia ikiwemo ya shilingi milioni 702 baina ya watumishi wa reli na serikali na ile ya maua rubibi wa kigoma dhidi ya wawakilishi wa kampuni ya tigo.
HIVI KARIBUNI WAFANYA KAZI 41 WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA WAMEISHINDA SERIKALI KATIKA KESI YA MAPITIO (REVISION) NAMBA 72 YA 2016 .KATI YA
ABDULLAH MABENGA & 40 OTHERS VS.RELI ASSETS HOLDING CO . LTD. (RAHCO)ILIYOKUWA IKIENDESHWA KATIKA MAHAKAMA YA KAZI KANDA YA DAR ES SALAAM AMBAPO MAHAKAMA IMEAMULU KUWA
WAFANYA KAZI HAO WALIFUKUZWA KAZI KINYUME NA TARATIBU NA RAHCO
IMEAMULIWA KUWALIPA WAFANYA KAZI HAO MILIONI MIA SABA NA MBILI. 702
WAFANYA KAZI HAO WALIKUWA WANAWAKILISHWA NA WAKILI MAARUFU THOMAS MSASA
KESI HII IMEAMULIWA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA NA JAJI Mashaka WA mahakama kuu KAZI Dar es salaam.
Kadharika MSASA amemsaidia mteja wake Maua Ramadhani Rubibi kushinda katika kesi yake ya madai dhidi ya kampuni moja iliyokuwa ikiwawakilisha kampuni ya mawasiliano ya Tigo ambapo mahakama ya kazi kitengo cha usuluhishi na upatanishi mkoani kigoma imempa maua ushindi na kutakiwa alipwe fidia ya zaidi ya milioni 30
Bi. Maua Rubibi mteja wa Wakili Msomi Thomas Msasa aliyeshinda kesi hivi karibuni
No comments:
Post a Comment