Ni kijana machachari, muhitimu wa shahada ya kwanza ya Biashara na Benk Katika chuo kikuu cha Dodoma.
kwa sasa ni kaimu katibu mkuu wa shirikisho la vyuo vikuu la chama cha mapinduzi, akijihusisha na ujenzi wa chama chake hicho anachokipenda na kukipigania tangu akiwa shuleni na baadae chuoni.
anaitwa Daniel Zenda, kijana makini, mtanashati , mcheshi na msikivu kwa vijana wenzake,
moja kati ya sifa kubwa ya Zenda ni utayari wake wa kukitumikia chama chake cha mapinduzi CCM bila kujali ujira atakaoupata kutokana na utumishi wake huo.
Daniel Zenda katika moja ya majukumu yake ya shirikisho la vyuo vikuu la chama cha mapinduzi hivi karibuni.
mara baada ya kuhitimu masomo yake chuo kikuu cha Dodoma UDOM, zenda alibahatika kupata ajira katika benki maarufu ya Barclays, lakini alifanya kazi muda mfupi sana na kuamua kuacha na kwenda kufanya shughuli za kujitolea CCM ili atimize ndoto yake ya kukitumikia chama anachokiamini.
akiwa CCM zenda amepata kuwa katibu msaidizi wa fedha wa wilaya, katibu msaidizi shirikisho la vyuo vikuu, na kwa sasa anakaimu nafasi ya ukatibu wa shirikisho hilo.
zenda amepata kufanya kazi na vijana mbali mbali ambao kwa sasa ni watumishi wa serikali wakiwemo Zainab Abdallah ambaye ni mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya pangani, Ally Salum Hapi mkuu wa wilaya ya kinondoni, Ngubiagai mkuu wa wilaya ya kilwa, Mtela mwampamba katibu tawala wa kisarawe na wengine wengi.
pichani wakuu wa wilaya Ally Hapi wa kinondoni na Zainab Abdallah wa Pangani walipokuwa watumishi wa shirikisho la vijana wa vyuo vikuu. katikati ni Daniel zenda wakielekezana jambo.
JAMVI LA HABARI linamtakia Zenda kila la heri katika utumishi wake ambaye kwa sasa anasimamia na kukamilisha chaguzi za uongozi wa matawi ya chama hicho katika vyuo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment