Manchester United watakutana na
klabu ya Saint-Etienne ya Ufaransa katika hatua ya 32 bora ligi ndogo ya
Ulaya, Europa League nao Tottenham Hotspur wakutane na Gent ya
Ubelgiji.
Kiungo wa Manchester United Paul Pogba atakutanishwa na ndugu yake mkubwa Florentin, anayechezea Saint-Etienne ambao kwa sasa wamo nambari nane Ligue 1.
Spurs hawajawahi kukutana na Gent, ambao walimaliza wa tatu ligi kuu ya Ubelgiji msimu uliopita.
Kwenye droo hiyo, klabu za Ligi ya Premia hazingepangwa pamoja, sawa na klabu kutoka taifa moja.
Fainali ya Europa League itachezewa uwanja wa Friends Arena mjini Stockholm mnamo 24 Mei.
Pogba vPogba
Kuhusu Paul Pogba kucheza dhidi ya kakake Florentin, 26, Mourinho alisema: "Ni jambo zuri. Paul atakuwa akicheka sana, na najua nduguye atakuwa anacheka pia. Ni jambo zuri, ambalo limefanyika mara chache sana katika historia ya soka."
Athletic Bilbao (Uhispania) v Apoel Nicosia (Cyprus) Droo kamili
Legia Warsaw (Poland) v Ajax (Uholanzi)
Anderlecht (Ubelgiji) v Zenit St Petersburg (Urusi)
Astra Giurgiu (Romania) v Genk (Ubelgiji)
Manchester United (England) v Saint-Etienne (Ufaransa)
Villarreal (Uhispania) v Roma (Italia)
Ludogorets (Bulgaria) v FC Copenhagen (Denmark)
Celta Vigo (Uhispania) v Shakhtar Donetsk (Ukraine)
Olympiakos (Ugiriki) v Osmanlispor (Uturuki)
Gent (Ubelgiji) v Tottenham Hotspur (England)
Rostov (Urusi) v Sparta Prague (Czech Republic)
Krasnodar (Urusi) v Fenerbahce (Uturuki)
Borussia Monchengladbach (Ujerumani) v Fiorentina (Italia)
AZ Alkmaar (Uholansi) v Lyon (Ufaransa)
Hapoel Beer Sheva (Israel) v Besiktas (Uturuki)
PAOK (Ugiriki) v Schalke (Ujerumani)
No comments:
Post a Comment