WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, December 7, 2016

LUKUVI ACHARUKA: AFUTA HATIMILIKI YA VIWANJA 15 VYA RAIA WA UINGEREZA KANDA YA ZIWA

William Lukuvi, waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (pichani)  amevifutia hatimiliki viwanja 15 vilivyokuwa vinamilikiwa na raia mmoja wa Uingereza ambapo serikali imevitaifisha viwanja hivyo vilivyopo katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Viwanja hivyo vilivyokuwa vinamilikiwa na Mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Hermant  Patel, mwenye uraia wa Tanzania na Uingereza kitendo ambacho ni kinyume na taratibu na sheria za nchini zinazozuia raia wa kigeni kumiliki ardhi.

Aidha, Mhe. Lukuvi amesema anayeruhusiwa kumiliki ardhi nchini ni raia wa Tanzania pekee na kuongeza kwamba kwa watanzania waishio nje ya nchi na kuukana uraia wao nao hawataruhusiwa kumiliki ardhi bali watapewa ardhi kama ilivyo kwa wawekezaji kutoka mataifa mengine.

Mhe. William Lukuvi amesema mtu akishaukana uraia wa Tanzania hana haki tena kama raia wa Tanzania, hivyo ataruhusiwa kumiliki ardhi kama mwekezaji tu na siyo kama raia wa Tanzania. 

Mhe. Lukuvi amesisitiza kuwa ardhi itabaki kuwa ya Watanzania tu na ameagiza mamlaka zota kutawasaka wale wote ambao wanamiliki ardhi kinyume na sheria za nchi.

Uamuzi wa kufuta hatimiliki hizo ulitolewa na Waziri Lukuvi wakati akizungumza na wanahabari juu ya hatua hiyo ya Serikali ya kuvifuta hati hizo jijini Mwanza. 

Lukuvi alisema kuwa awali Serikali ilikuwa ikifahamu mfanyabiashara huyo ana hatimiliki ya viwanja vitano lakini baada ya uchunguzi uliohusisha Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza wamebaini raia huyo anamiliki jumla ya viwanja 15.

No comments:

Post a Comment