Mwenyekiti
wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda kulia
akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam mara
baada ya kupata uongozi mpya wa kampuni hiyo ulioteuliwa rasmi hivi
karibuni na bodi ya NICOL kushoto ni Mtendaji Mkuu Bw. Adam Wamunza. Picha Na Ally Daud-Maelezo
Na Ally Daud-MAELEZO
Kampuni
inayojihusisha na uwekezaji nchini (NICOL) imejidhatiti kuendeleza
uwekezaji wa hisa nchini ili kukuza uwekezaji wa ndani na kuleta
ushindani kwa wawekezaji ndani na nje .
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw.
Gideon Kaunda wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo
jijini Dar es salaam.
“Sasa
tunahitaji kuendeleza uwekezaji wa ndani katika hisa na hivi karibuni
tumenunua hisa ili kukuza uwekezaji na kuleta ushindani kwa wawekezaji
wa nje katika soko huria” alisema Bw. Kaunda.
Aidha Bw.
Kaunda amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanapata wawekezaji wa
ndani ili kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuweza kuleta ushindani .
Mbali na
hayo Bw. Kaunda amesema kuwa wanataraijia kuwekeza kwenye sekta zote za
uchumi kama mazao ya biashara ikiwamo korosho,gesi, mafuta pamoja na
madini ili kuweza kutangaza bidhaa za Tanzania kwenye soko la nje.
Aidha Bw.
Kaunda aliwataka wawekezaji wote wa ndani na wa nje kushirikiana na
NICOL katika shughuli za uwekezaji hasa wa mazao ya biashara ili
kuipeleka Tanzania katika soko la kimataifa kwa manufaa ya kizazi cha
sasa na kijacho.(P.T)
No comments:
Post a Comment