Riek Machar anaedaiwa kuzuiliwa Afrika Kusini
Shirika la habari la Reuters limesema vyanzo vya kidiplomasia na
kisiasa vimesema Jumanne kuwa kiongozi wa uasi Sudan Kusini Riek Machar
alietorokea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Agosti baada
ya mapigano makali ameshikiliwa Afrika kusini ili kumzuia kuzua vurugu
tena.
Zaidi ya watu milioni moja wametoroka Sudan Kusini tangu mapigano
yalipoanza 2013 baada ya Rais Salva Kirr kutoka kabila la Dinka
alipomfuta kazi Machar anaetoka kabila la Nuer kama makamu wake.
Kiongozi mmoja wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa kutoka Afrika
kusini amesema Machar amezuiliwa nyumbani katika mji wa Pretoria wakati
mienendo yake akifautiliwa kwa karibu na pia mawasiliano yake kwa njia
ya simu kunaswa.
No comments:
Post a Comment