WILAYA
ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imeelezwa kuendelea kuporomoka kiuchumi kutokana na mzunguko mdogo wa fursa za kibiashara kupelekwa wilaya ya jiran na watumishi wa idara inayohudumia wakimbizi katika kambi ya mtendeli kuishi Wilayani Kibondo, hali inayo pelekea shughuli zao zote kufanyika Wilayani humo.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagala alitoa wito kwa watumishi hao kutoa fursa za kiuchumi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kakonko wakati wa ujenzi wa nyumba za kudumu za wakimbizi, lengo likiwa ni kuongeza mzunguko wa kibiashara
kwa Wananchi wanao izunguka kambi hiyo na kuacha tabia ya kutoa tenda zote za ujenzi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kibondo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani humo, Ndagala alisema watumishi
wengi wa Kambi ya mtendeli wamekuwa wakifanya biashara na wafanya biashara wa Kibondo,wakati kambi hiyo inahudumia wakimbizi katika Wilaya ya Kakonko hali inayo pelekea uchumi wa wananchi wa Kakonko waliotegemea kuupata kupitia kambi hiyo kuanzishwa kukosekana na kuhamia wilya nyingine ya Kibondo.
Ndagala alisema halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ni halmashauri ambayo uchumi wake bado upo chini,unahitaji kuinuliwa hivyo akawaomba wafanyakazi wa kambi ya Mtendeli pamoja na
shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoa vipaumbele kwa Wananchi wa Wilaya ya Kakonko ili kuinua uchumi wa Wilaya hiyo kwa kuwapatia ajira za ujenzi na ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa wafanya biashara wa Kakonko.
Hata hivyo Mkuu huyo aliwaomba watumishi wote wa Kambi hiyo na mashirika yanayo hudumka wakimbizi kurudi kuishi Kakonko kwakuwa sababu iliyo kuwa ikiwapelekea waishi Kibondo ya kukosekana kwa Nyumba za kupanga Wilayani humo limekwisha Wananchi wamejitahidi kujenga nyumba zenue ubora ambazo wanaweza kupanga na kufanya kazi zao za kuhudumia wakimbizi wakiwa wilayani humo.
No comments:
Post a Comment