WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Monday, December 5, 2016

ADVOCATE MSASA:- WAKILI KIJANA ANAYEPENDWA NA WENGI KIGOMA NA TABORA

Wakili Thomas Msasa..

''nilipohitimu chuo kikuu na kufanikiwa kumaliza shule ya sheria, nilifanya kazi ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa muda kidogo, baadae nikaamua kurudi nyumbani kusaidia wananchi wenzangu wa Kigoma kuwapatia msaada wa sheria''. alisema wakili kijana Matatizo Thomas Msasa anayetambulika pia kwa jina la Nyerere kutokana na tabia yake ya kutembea na fimbo.

msasa ni miongoni mwa mawakili vijana maarufu zaidi mkoani kigoma kutokana na kesi kadhaa alizowahi kuwatetea wananchi mbalimbali nyingine kwa kujitolea bila malipo lengo lake likiwa ni kuwafanya hata masikini nao wapate haki zao.

''najua huku mikoani hasa mikoa ya pembezoni kama kigoma, kuna malalamiko mengi sana ya ardhi, watu wanaonewa sana na kwa kukosa kwao watetezi wanashuhudia haki zao zikipotea na kuishia kulia''. aliongeza msasa.

Msasa amesema watanzania wote na wanakigoma wenye matatizo ya kisheria anawakaribisha wamuone ili awapatie msaada wa kisheria kwa kadri ya uwezo wake kwa kupigia simu namba 0759736418

hivi karibuni wakili msasa alimtetea mfanyabiara Amiri Kirungi wa Kirungi Kingalu Limited aliyekuwa anakabiliwa na kesi inayohusiana na masuala ya misitu akishitakiwa na serikali ya mkoa wa tabora, kesi ambayo waliibuka kidedea Msasa na mteja wake kingalu.

kwa sasa Msasa amefungua kampuni yake ya kiwakili inayoitwa TABORA LAW CHAMBERS

No comments:

Post a Comment