WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, January 3, 2017

BREAKING NEWS: WAHAMIAJI HARAMU WAJIFICHA KWENYE BRIEFCASE


Maafisa wa polisi wa Cueta walichapisha picha hii siku ya JumapiliPICHANI HAWAMIAJI HARAMU WAKIWA KATIKA BRIEFCASE KAMA NGUO.

Maafisa wa polisi wamewakamata raia wawili wa Morocco ambao walijaribu kuwaingiza wahamiaji katika eneo linalotawaliwa na Uhispania lililo kazkazini mwa Afrika la Cueta- wawili hao wakiwa wamejificha ndani ya gari na mwengine katika sanduku.
Wakati maafisa wa polisi walipokagua gari moja siku ya Jumatatu ,mtu mmoja alipatikana amefichwa katika eneo la mbele la gari na mwengine amefichwa katika eneo la kiti cha nyuma cha gari.
Mwanamume huyo na mwanamke ,wanaodaiwa kuwa raia wa Guinea ,walipata huduma ya kwanza kwa kuwa walikuwa na hewa kidogo ya kupumua.Mtu mwengine alipatikana amefichwa katika eneo la gari la mbele maarufu dashboardMtu mwengine alipatikana amefichwa katika eneo la gari la mbele maarufu dashboard

Kwengineko kijana mmoja wa asili ya Kiafrika alipatikana amefichwa katika sanduku la mwanamke.
Kisa hicho kilitokea mnamo mwezi Disemba 30 na mtu huyo anayeaminika kutoka Gabon alihitaji matibabu ya dharura.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 kutoka Morocco alijaribu kumuingiza Cueta, lakini maafisa wa uhamiaji walimuagiza kufungua sanduku lake ambalo lilikuwa limefungwa katika kitoroli.
Kisa hicho kinajari wakati ambapo kumekuwa na jaribio la wahamiaji wengi kuvunja ua wa mita sita unaogawanya Cueta na Morocco.Mwengine alipatikana amefichwa chini ya kiti hiki kilichotengezwa ili kumtoshaMwengine alipatikana amefichwa chini ya kiti hiki kilichotengezwa ili kumtosha
Raia 50 wa Morocco na 5 wa Uhispania walijeruhiwa wakati wahamiaji 1,100 walipojaribu kupita ua huo na kuingia Cueta kutoka Morocco.
Hakuna aliyefanikiwa kupita ,lakini watu wawili walijeruhiwa walipokuwa wakivunja ua huo na kupelekwa hospitalini huko Ceuta.
Mlinzi mmoja alipoteza jicho lake kulingana na maafisa.
Kisa kama hicho mnamo tarehe 9 Disemba kilihusisha zaidi ya wahamiaji 400 kutoka Afrika.
BBC

No comments:

Post a Comment