WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, January 25, 2017

MGOGORO CUF : NANI YUPO SAHIHI?. PIGA KURA YAKO TUONE

Kwa muda kadhaa sasa kumekuwepo na sintofahamu na kurushiana maneno kwa hapa na pale baina ya pande mbili ama tatu. upande wa CUF unaoongozwa na Seif Sharrif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho,
Tokeo la picha la maalim seif
Maalim Seif Sharrif Hamad
upande mwengine ni wa Prof. Ibrahim Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho ambaye hapo awali alijiuzulu na katikati mwaka jana aliamua kurejea kitini kwake. na mwisho
Tokeo la picha la lipumba
Prof. Lipumba
ni upande wa serikali kupitia msajili wa vyama vya siasa ambaye yeye anasema anawatambua wote wawili kama viongozi halali wa chama hicho.

Tokeo la picha la jaji mutungi
Jaji Fransis Mutungi, Msajili wa vyama vya siasa

UPIGAJI WA KURA.
ili kupata maoni ya watanzania mbalimbali wanachama wa chama hicho na wasio wanachama, Jamvi La Habari tumeanzisha upigaji huru wa Kura utakaodumu kwa muda wa siku kumi.

namna ya kupiga Kura, ingia katika blog yetu hii ya Jamvi la habari ambayo ni www.jamvilahabari1.blogspot.com, 
kisha upande wako wa kulia juu utaona kona ya maswali inayokutaka kuchagua jibu moja tu.
kila siku tutakuwa tunatoa mrejesho wa nani yupo sahihi katika sakata hili kwa kadri ya kura zitakavyokuwa zinapigwa.

shiriki sasa kuupigia upande unaouona ni sahihi. 

No comments:

Post a Comment