Donald Trump asema kwamba Korea
Kaskazini haitafanikiwa katika mpango wake wa kuunda kombora la masafa
marefy litakalofika Marekani.
Rais mteule wa Marekani, Donald
Trump, amepuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora
linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi Marekani.
Katika
mawasiliano kupitia mtandao wa Twitter, Bwana Trump aligusia majigambo
ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka
mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia
hatua ya mwisho.
Bwana Trump alisema katika ujumbe wake kuwa
"Haitawezekana." Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa
sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina
uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.
Ujumbe wa Twitter wa bwana Trump.
Bwana Trump pia alishutumu Uchina kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake
Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea pesa kiasi kikubwa
cha pesa na mali kutoka Marekani
BBC
No comments:
Post a Comment