Godbless Lema Arudishwa Tena Gerezani.....Ni Baada ya Serikali Kuwasilisha Notisi Ya Kupinga Dhamana yake Mahakama ya Rufaa
Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi
ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya
mawakili wa Serikali kuwasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama
ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi alitarajiwa kutoa
uamuzi juu ya rufaa ya Jamhuri iliyopinga Lema kupatiwa dhamana Novemba
11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha
katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya
Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri iliwasilisha notisi ya
mdomo.
No comments:
Post a Comment