WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, January 25, 2017

CUF WAZIDI KUZODOANA

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA VYOMBO HABARI
Imetolewa leo Tarehe 19/1/2017
Na kurugenzi ya Habari,
Tokeo la picha la lipumba na seif
Kumekuwapo na UPOTOSHAJI mkubwa wa makusudi kuhusu Chama Cha wananchi Cuf kupatiwa RUZUKU yake na Ofisi ya Msajili.
Mwanzo Upotoshaji ulifanywa na Ndugu MTATIRO kupitia PRESS yake na wandishi wa Habari na maandiko yake mbalimbali katika mitandao ya kijamii.

Kupitia Kurugenzi yangu tulitoa ufafanuzi wa kina kuhusu swala hili na kujibu karibu hoja zote za Ndg MTATIRO.

Kwa masikitiko makubwa ameibuka Ndg Mbarala MAHARAGANDE na yeye kaja na hoja ile ile lakini katika mtindo wa kumtukana na kumdhalilisha Msajili wa vyama.
Kilicho tufanya kujibu hoja za Ndg MAHARAGANDE ni upotoshaji wa vifungu vya Katiba ya Chama Chetu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Cuf ya Mwaka 1992 Toleo 2014 Imeeleza kila kitu kuhusu mambo ya fedha na madaraka ya viongozi. Katiba ya Cuf ipo wazi na kwa makusudi Maharagande ambae leo anajiona kua ni Msafi ameshindwa kuonyesha Ibara ya Katiba ya Cuf au kifungu kilichokiukwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mtungi. Katiba ya Cuf imeeleza wazi kazi za Katibu Mkuu kupitia lbara ya 93 (a) mpaka (k) lakini pia kifungu cha 2 na 3. Kazi za Katibu Mkuu ni pamoja na masuala ya usimamizi wa Fedha ambayo ipo katika kifungu (i) ibara hiyo ya 93 hakuna ubishi katika hilo, lakini ni vizuri Watanzania wakaelewa kwamba, kwa mujibu wa Katiba hii, kifungu cha 3 ibara hiyo hiyo ya 93 ambayo inaeleza Kazi za Katibu Mkuu inasema,

nanukuu
Katibu Mkuu atakapokua Nje ya Nchi au atakaposhindwa kufanya kazi zake kwa sababu yoyote ile, Naibu Katibu Mkuu anaemfuatia kwa madaraka atakua Kaimu Katibu Mkuu hadi pale Katibu Mkuu atakapokua tayari kuendelea kutekeleza Majukumu yake.

Mwisho wa kunukuu, katika hali hii ambayo Katibu Mkuu ambayo Katibu Mkuu amesusa kufika Ofisini kwa sababu anazozijua yeye, Sakaya ana kua ndie Kaimu Katibu Mkuu na anatekeleza majukumu ya Katibu Mkuu likiwemo lile la Fedha. Lakini hawa jamaa Wanaojiita Viongozi

No comments:

Post a Comment