WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, January 25, 2017

MADAWA MICHEZONI: Usain Bolt kupokonywa dhahabu moja

Usain Bolt na Nesta CarterUsain Bolt na Nesta Carter.

Bingwa wa mbio za mita 100 upande wa wanaume Usain Bolt atalazimika kurudisha dhahabu moja miongoni mwa dhahabu tisa alizoshinda baada ya mwanariadha mwenza Nesta Carter kupatikana alitumia dawa za kusisimua misuli.

Carter alikuwa miongoni mwa wanariadha wanne wa Jamaica walioshinda mbio za mita 100 kupokezana vijiti katika michezo ya beijing 2008.
Ni miongoni mwa wanariadha 454 waliochukuliwa violezo vyao na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC mwaka uliopita na amepatikana alitumia dawa ya aina ya methylhexaneamine.
Bolt mwenye umri wa miaka 30 alishinda dhahabu tatu katika michezo ya Olimpiki ya Rio msimu uliopita.

Alishinda dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 400 kupokezana vijiti na kuongeza mafanikio yake katika mbio hizo mwaka 2008 na 2012.
Carter mwenye umri wa miaka 31 alikuwa miongoni mwa wanariadha walioshinda dhahabu katika mbio hizo mjini London miaka mitano iliopita na kuisadidia Jamaica katika mbio za dunia miaka ya 2011, 2013 na 2015.

Alikuwa wa kwanza kukimbia katika mbio za rilei za 4 mara 100 mjini Beijing ambazo zilimuhusisha mwanariadha Michael Frater, Asafa Powell na Bolt.
Jamaica ilishinda kwa kuvunja rekodi ya dunia baada ya kumaliza kwa sekunde 37.10 mbele ya Trinidadad and Tobago na Japan ,ambao sasa medali zao zitaongezwa.
Brazil itajipatia medali ya shaba.

No comments:

Post a Comment