WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, January 4, 2017

WATU WATU WATATU WANUSURIKA KUUWAWA KUFUATIA TUKIO LA UJAMBAZI MKOANI KIGOMA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMr5FG0Md2yCM2YIl9B4Rkp94FmPBYmuehLHoPmFVPNIU5G4G1OLSHB62HWL6_4xDULp8KfapoJ67x_Hrsjudg48L19xfU5V13TEo0SA1QzGrPAbaccLW9d6jZ9G-dzDR8WUIvDD3xKJo/s1600/WhatsApp+Image+2017-01-04+at+13.31.32.jpeg

 Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WATU
watatu wamenusurika kufa Mkoani Kigoma katika tukio la Unyang'anyi wa kutumia silaha lililotokea katika eneo la Zuru Manispaa ya kigoma ujijj ambapo Majambazi sita wasio julikana wakiwa na silaha aina ya SMG/SAR 01walivamia Duka la Mpesa la Mfanya biashara ,Hussen Issa  na Kuiba Kiasicha shilingi 250,000 pamoja na simu tatu .

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Wa Kigoma, alisema mnamo tarehe
3 Januari mwaka huu majira ya saa 20:30 usiku Huko zuru Gungu  Watu sita wasio faamika waliingia dukani kwa mfanya biashara huyo kama wateja hukuwakiwa wameficha siraha zao kwenye makoti baada ya Wizi huo kufanyika waliwapiga Risasi watu wa tatu katika vurugu za kufanya Wizi huo.

Mtuialiwataja walio jeruhiwa na Risasi hizo ni Hamad Kharid (36) alipigwa ubavuni ,Hussen Ndoroma (42) amejeruhiwa maeneo ya makalio na Sifa  Salimu (65)  amejeruhiwa na risasi miguuni ambapo risasi hiyo ilimkuta Nyumbani kwake ambapo ni jirani na wafanya biashara hao.

Aidha Mtui alisema Mpaka sasa majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa Maweni na Jeshi la polisi linawashikilia watu wawili kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo na msako mkari unaendelea kuwasaka majambazi hao wanaofanya matukio hayo ya Unyang'anyi kwa kutumia siraha.

"NiwaombeWananchi  kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi dhidi ya  uhalifu ilikuunga mkono jitihada za kuondoa uhalifu kwa kutoa taarifa za waalifu wanao jihusisha na vitendo vya kiuhalifu ilihatua za kisheria ziwe zinachukuliwa dhidi yao", alisema Mtui.

Kwa Upande wake Majeruhi wa tukio hilo, Hussen Ndoroma alisema jana majira ya saa moja
usiku kuna watu ambao walifika dukani kwake wakiwa waneshika panga na wengine siraha ya SMG baada ya kubishana nao ndipo walipo amua kumpiga Risasi ya Mguuni iliyotokea  kwenye makalio ndipo ilipoenda kumpiga  Mwanamke mmoja aliekuwa Nyumba kwake.

Alisema majambazi hao walifanikiwa kuchukua kisasi cha shilingi 250,000  pamoja na simu tatu
na kuingia duka la Mwenzake  Ahmadi Kharid aliekuwa akiomba msaada mwenzake asaidiwe ndipo walipo mpiga risasi eneo la ubavu wa Kushoto.

Hata hivyo Sifa Salim ambae pia nae ni miongoni mwa majeruhi hao alisema  Yeye akiwa Nyumbani kwake maeneo ya zuru akiendelea na Shughuli zake za nyumbani alishtukia kitu kinakuja na kumpiga maeneo ya miguuni na kushtukia damu zikiendelea kitoka hakujua tatizo ninini.

Nae Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni Fadhiri Kibaya 
alikili kupokea majeruhi hao wakiwa katika hali mbaya na majeraha yao yaki vuja damu kwa Wingi ndipo walipo wachukua na kuanza kuwafanyia matibabu , mpaka sasa hili zao ni nzuri na wagonjwa wanaendelea na mayibabu.

No comments:

Post a Comment