WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Sunday, January 22, 2017

NJAMA ZA KUMCHAFUA JAJI MUTUNGI ZAVUJA: WABUNGE KOMU NA KUBENEA WA CHADEMA WATUMIA GAZETI LAO KUFANIKISHA

  • MWANAHALISI LAPANGWA KUTUMIKA
  • LADAIWA KUOKOTEZA USHAHIDI KUMCHAFUA
  • LENGO ALEGEZE MSIMAMO SAKATA LA CUF.
 mkakati maalum umepangwa ili kumtisha, kumchafua na kumdharirisha msajili wa vyama vya siasa jaji Fransis Mutungi kupitia Gazeti la kila wiki linalomilikiwa na wabunge wa chadema Anthony Komu wa moshi vijijini na Saed Kubenea wa Ubungo la mwanahalisi taarifa za ndani za gazeti hilo zinaeleza.

mpaka sasa taarifa zinasema, msimamo wa Jaji Mutungi kuhusiana na kusimamia ipasavyo sheria ya vyama vya siasa na katiba ya CUF katika kutatua mgogoro wa kiuongozi wa ndani ya chama hicho, umewachanganya viongozi wengi wa CHADEMA na wale marafiki wao wa CUF-Maalim Seif kiasi cha kuamua kumchafua Msajili huyo kama njia ya kumtisha na kumrudisha nyuma.

taarifa za uhakika zinasema uchafuzi huo wa kitaswira unafanana na ule ambao gazeti hilo liliwahi kuwafanyia Zitto Kabwe, Edward Lowassa, Fransis Mbatia na wanasiasa wengine kwa kutekeleza kile kinachoitwa (Character Assasination)
WAKATI taarifa za kuvuja huko kwa mbinu mpya za kumkabili na  kupambana na Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Fransis Mutungi zinazohusisha matusi, kejeli, na kumuhusisha msajili na ofisi yake na tuhuma za kila aina ili pengine abadili msimamo, mbinu zinazopangwa na wanaojiita kamati ya Uongozi ya chama cha CUF ambayo Ofisi ya Msajili haiitambui kamati hiyo na kusisitiza kumtambua Lipumba kama mwenyekiti na Maalim Seif kama Katibu mkuu.
Tokeo la picha la KUBENEA
Mmiliki wa Gazeti la Mwanahalisi ambaye pia ni Mbunge wa ubungo Chadema, Saed Kubenea
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili, imezipata ni kwamba tayari mbinu hizo zimeanza kutekelezwa na viongozi wa kamati hiyo kwa kuanzia na kusambaza habari zinazomdhalilisha msajili wa vyama katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii nchini.

Moja kati ya mkakati huo ni ile iliyosambazwa juzi na Mbarala Maharagande taarifa iliyojaa kejeli, matusi, tuhuma na dhihaka kwa msajili wa vyama vya siasa na kuacha kujibu hoja za msingi ambazo awali zilitolewa na ofisi ya msajili.

Akizungumzia taarifa hizo, Jaji Mutungi alisema kwamba yeye haogopi kuchafuliwa kwa aina yoyote kwa kuzingatia ukweli kwamba yeye ni mtumishi wa umma na anafanya kazi zake kuutumikia umma kwa mujibu wa sheria za nchi na kamwe hawezi kuyumbishwa na matusi wala kejeli zozote zinazotolewa dhidi yake na ofisi yake.

"Namimi nimezipata hizo taarifa kwamba kuna baadhi ya watu wamepanga kupambana nami kwa kunichafua, japo naendelea kuzifanyia kazi lakini kwa kifupi kabisa niwaambie waache wanichafue na wala siogopi lolote". alisema.
Tokeo la picha la anthony komuMmiliki mwenza wa Mwanahalisi ambaye pia ni Mbunge wa Moshi vijijini CHADEMA. Anthoyn Komu

"Mimi ni mtumishi wa umma na ninafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo siwezi kuyumbishwa na mambo ya kitoto hayo ya kuchafuana na kurushiana tuhuma zisizo na kichwa wala miguu. Sidhani kama kumshambulia Mutungi kunaweza kuleta tija ya wao kufikia malengo yao". alisema.

Aidha, alisema mjadala wa ruzuku ya CUF aliyotoa kwa Chama hicho ameshaufunga na anashangazwa na maneno ya hayo uongo yanayozidi kusambazwa na watu wanaojiita viongozi wa CUF.

Jaji Mutungi  alisema yeye ni muumini haki na sheria, na ndio maana mamlaka za uteuzi zilimuamini na kumpa nafasi ya Ujaji.

"Natambua uadilifu wangu na sitaki niuelezee, ila nahisi tukiendelea kulizungumzia hili tutakuwa tunalikuza bila sababu za msingi. Nasisitiza tena kuwa ofisi yangu inamtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu,''alisema.

Kutokana na hali hiyo, alisema kinachoendelea kufanywa na kundi la watu wanaojiita viongozi wa CUF kuzungumza mambo mengi ya uongo na kumuhusisha yeye  bila ukweli huku wakishindwa kuisoma vyema Katiba yao wenyewe inayowaongoza.

"Nasisitiza tena si Mutungi au Ofisi ya Msajili iliyoandika Katiba ya CUF, ni wao wenyewe wameiandika. Ofisi ilichofanya ni kuitafsiri katiba yao wenyewe na kutoa muongozo. Sasa tatizo liko wapi?''alisema.

Taarifa za ndani ya mkakati huo zinasema pamoja na mitandao ya kijamii,  yamepangwa pia kutumika magazeti kadhaa likiwemo gazeti moja maarufu la kila wiki linalotoka siku ya jumatatu linalomilikiwa na abunge wawili wa Chama kimoja cha upinzani hapa nchini.

Hivi karibuni, mtu anayejiita Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Mbarala Maharagande alizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ofisi ya Msajili inasababisha mpasuko ndani ya chama hicho na ndio maana imetoan ruzuku kwa Lipumba.

JAMVI LA HABARI lilibua namna SHILINGI milioni 369 zilizodaiwa kutoroshwa kutoka hazina na kwenda katika
akaunti ya Chama cha CUF wilaya ya Temeke, Januari  5 na baadae kugawanywa  kwa
watu mbalimbali, zinaelezwa ziliingizwa kihalali kwa kufuata sheria na
taratibu zote za kiofisi kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jamvi la Habari linaweza kuthibitisha.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya chama cha wananchi CUF
ambaye ofisi ya  msajili wa vyama vya siasa haimtambui, Julius Mtatiro
alikaririwa na vyombo kadhaa vya habari akilalamikia juu ya alichokiita
kuchotwa kwa fedha za ruzuku za chama hicho kitendo alichokiita kupewa
baraka na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata, zinaonyesha kuwa hakukuwa
na tatizo lolote la kisheria, kimaadili wala kikanuni katika utoaji wa
fedha hizo ambazo ni sehemu ya fedha za ruzuku ambazo CUF wanastahili
kupata kutoka serikali kuu kwa shughuli za uendeshaji wa chama hicho.
Tokeo la picha la mutungi
Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Fransis Mutungi.

Taarifa hizo zinasema zaidi kuwa sio kweli fedha hizo ziliingizwa katika
akaunti ya wilaya ya Temeke isipokuwa kwa sasa, Temeke ni jina tu la
akaunti hiyo kama ambavyo akaunti nyingine zinaitwa Holland, Vijana,
Kijitonyama na kadharika, na kwamba akaunti hiyo ni halali na imehuishwa
kwa kubadilishwa matumizi yake kutoka kuwa akaunti ya wilaya mpaka kuwa
akaunti maalum ya taifa kwa kufuata vikao halali vya mashauriano ya chama
hicho.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu aliye ndani ya serikali, anasema ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa ilipata uthibitisho pasi na shaka kwamba  akaunti
hiyo ni halali kwa kukipatia chama hicho ruzuku yao kama walivyoomba
viongozi waandamizi wanaofahamika na kutambulika na msajili wa vyama.

‘’Unajua msajili hajajiingizia tu zile fedha, CUF wenyewe walileta maombi
kuwa fedha zao kwa sasa ziingizwe katika akaunti namba fulani inayopatikana
sehemu fulani, ndipo msajili alipofuatilia na kuwataka watimize masharti
yote ya kikatiba ikiwemo kufuata vikao halali vya chama chao na kuwaingizia
fedha hizo baada ya kuombwa muda mrefu kufanya hivyo’’. Kilisema chanzo
chetu

‘’Ukweli ni kwamba Msajili anaifahamu CUF moja tu,  msajili yeye haifahamu
kamati inayoongozwa na Mtatiro na wenzake, anachofahamu msajili wa vyama
vya siasa kuwa kuna CUF, ambacho Mwenyekiti wake ni Profesa Ibrahim
Lipumba, Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharrif Hamad, na manaibu wake
Magdalena Sakaya na Nassoro Mazrui kila mmoja’’ kiliongeza chanzo chetu.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa  kitendo cha
Profesa Lipumba kumtambua na kuwa tayari kufanya kazi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kimempa moyo msajili kuwa akuwapatia ruzuku kina Lipumba kutapelekea kazi za chama kizima kufanyika kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akimuita ofisini katibu mkuu wake
kumpangia kazi za kufanya.

Tofauti na Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif, ambaye ameendelea kusisitiza
kutomtambua Mwenyekiti wake Lipumba, bila kujali ukweli kwamba mamlaka
iliyomchagua haikuwahi kurudhia kujiudhulu kwake.

"katika akili tu ya kawaida, mwenyekiti wa chama ndio kiongozi mkuu wa
shughuli za kichama katika CUF, yeye anathibitisha anamtambua Katibu Mkuu
wake na yupo tayari kushirikiana naye kufanya kazi, Katibu Mkuu yeye hataki
kumtambua na anaendelea kuing’ang’ania Kamati ya Uongozi ambayo kisheria
haitambuliki, unafikiri ili chama kiendelee kupewa ruzuku na kijiendeshe,
nani angepewa ruzuku kama si Lipumba’’.  Alisema Chumi Kisyabo aliyeombwa na gazeti hili kutoa maoni yake.

‘’Kwa maoni yangu, kumpa ruzuku Lipumba ni kukifanya chama chao kiende
mbele kwa kuwa Lipumba ndio kiongozi mkuu wa chama na anawatambua wasaidizi wake wote halali akiwemo Maalim Seif, na kumpa ruzuku Maalim Seif ni kukidumaza chama na kuchochea  mgogoro kutokana na msimamo wa wake wa kutomtambua, kwa hili namuona msajili wa vyama kama mtu aliyetumia akili nyingi sana kuutatua mgogoro huu’’. Alisema.

Sakata la ruzuku la chama hicho kimeendelea kuchukua nafasi katika vichwa
vya habari mbalimbali ambapo jumapili ya Januari 15, 2017 anayejiita
Mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama hicho, Mtatiro alishiriki kwa njia
ya simu mjadala kuhusu jambo hilo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano
kwa Umma, Abdul  aliyekuwepo studio katika kituo cha Star Tv jijini Mwanza
na wawili hao kushindana kwa hoja, katiba na uzoefu wao ndani ya chama
hicho huku kambaya akimtuhumu mtatiro kuwa ni mpiga madili mzoefu.

‘’Namshangaa Julius(Mtatiro) leo analalamika sisi kuingiza  fedha hizi
kwenye akaunti ya diwani wetu na anasema ni wizi, wakati yeye mwaka 2011
aliingiziwa milioni mia moja na nane (108) katika akaunti yake binafsi ,
sasa leo analalamika nini nay eye mwenyewe aliwahi kumuingizia diwani huyo
huyo milioni 46’’?. Alisema Kambaya.

Katika majibu yake,  Mtatiro alikiri kuingiziwa na kusema ziliingizwa
kwababu ya kampeni za uchaguzi mdogo igunga, japo akaunti ya wilaya hiyo ya
igunga ilkikuwepo.

Katika hatua nyingine kiongozi mwandamizi wa chama hicho na mbunge maarufu mstaafu  wa Mkanyageni, Habib Mnyaa alipiga simu studio hizo na kusema yeye kama mwanachama na kiongozi mwandamizi wa chama hicho haoni shida kwa wao kuingiziwa fedha kwenye akaunti hiyo kwa kuwa ni akaunti halali ya chama na kwamba kuziingiza kwenye akaunti binafsi ya mtu ni jambo la chama ambalo halihusiani na msajili wa vyama.

"Msajili hajaingiza fedha kwenye akaunti ya mtu binafsi, msajili ameingiza
fedha kwenye akaunti ya chama, na kwa hivyo hakuna tatizo lolote kisheria,
chama kimetumiaje hizo fedha ndio swala linaloweza kuibua mjadala, na hata
hivyo mamlaka ya ubadhilifu sio ya mtatiro ni mamlaka ya CAG, hivyo hatuna
haja ya kuwa na papara, tusubiri tuone matokeo ya msajili, kwenye hili
Msajili hana makosa na ninampongeza sana kwa kweli’’. Alisikika Mnyaa.

No comments:

Post a Comment