WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, January 3, 2017

EXCLUSIVE NEWS : FANYENI KAMPENI ZA KISTAARABU NA KUFUATA SHERIA ZA NCHI - JAJI MUTUNGI


. http://swahilitimes.com/wp-content/uploads/2016/08/Jaji-Francis-Mutungi.jpgJaji Fransis Mutungi Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini.
Msajili wa vyama vya siasa jaji Fransis MUTUNGI amevitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki chaguzi ndogo za marudio zinazoendelea sehemu mbalimbali  hapa nchini kufanya kampeni za kistaarabu huku wakijikita kwenye kunadi Sera zao na kuwasisitiza waendelee kuliunganisha taifa na sio kushambuliana baina ya vyama wala vyama na serikali.
Jaji Mutungi ameyasema hayo Leo wakati akitoa salamu maalum za mwaka mpya kwa vyama vya siasa na watanzania wote.
"Unajua siasa na wana siasa lazima wakomae sasa,  siasa za kizamani zilikuwa hazinogi kama hakuna kurushiana vijembe, kejeri na Matusi.  Sasa hivi mambo hayo yameshapitwa na wakati na wanasiasa hasa wanaowanadi wagombea wao wahakikishe wanatumia Muda mwingi Zaidi kunadi sera zao kuliko kushambuliana". Alisema Mutungi  
''...unajua siasa.......siasa za chuki zinazogubikwa nakurushiana vijembe....zimeptwa na wakati....''liongeza Jaji Mutungi 
JAMVI LA HABARI lilipotaka kujua ni nini ofisi yake inawaahidi watanzania na wafuatiliaji wa siasa kwa mwaka huu mpya 2017 tuliouanza juzi, Jaji Mutungi ameahidi kuendelea kutoa huduma Sawa kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini kwa kuwa ofisi yake ina wajibu wa kuvilea vyama hivyo na Demokrasia. ...
kadharika jaji mutungi ameahidi kuendelea kudumisha ukuaji wa demokrasia nje na ndani ya vyama na kuvikumbusha  vyama kujiendesha kama taasisi na kuhimiza vyama kufuata katiba zao na si matakwa ya Viongozi pasipo kuzingatia matakwa ya katiba zao.
nakala ya Calender ya mtandaoni iliyotolewa na msajili wa vyama vya siasa

No comments:

Post a Comment