WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Monday, January 16, 2017

Korea Kusini: Mwendesha mashtaka ataka mkuu wa Samsung akamatwe

Lee Jae-yongLee Jae-yong amekuwa akisimamia Samsung tangu babake alipougua mwaka 2014
Mwendesha mashtaka maalum nchini Korea Kusini anaitaka mahakama itoe kibali cha kukamatwa kwa mkuu wa kampuni ya Samsung kutokana na mchango wake katika kashfa ya ufisadi nchini humo.

Msemaji wa afisi ya mwendesha mashtaka Lee Kyu-chul amesema Lee Jae-yong alilipa zaidi ya dola 35 milioni za Marekani kwa nyakfu zinazoungwa mkono na Choi Soon-sil, rafiki wa Rais Park Geun-hye.
Mwendesha mashtaka huyo anasema pesa hizo zilikusudiwa kuhakikishia uungwaji mkono wa mpango wa kuunganisha kampuni mbili zilizohusishwa na Samsung.

Bw Lee amekanusha tuhuma hizo. Samsung haijatoa taarifa yoyote kufikia sasa.
Bw Lee, anayefahamika kama Jay Y Lee, alihojiwa kwa zaidi ya 20 na maafisa wa mashtaka mjini Seoul wiki iliyopita.
Kwa sasa ni naibu mwenyekiti wa Samsung Electronics, lakini tangu babake, Lee Kun-hee, alipopata mshtuko wa moyo mwaka 2014, amekuwa akitazamwa kama mkuu wa kampuni hiyo.
Kashfa hiyo inatishia kumtoa madarakani Bi Park ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi mwa muda Mahakama ya Juu inapoendelea kuchunguza tuhuma dhidi yake na mswada wa kumuondoa madarakani.
BBC

No comments:

Post a Comment