Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kuwa umefurahishwa na
kitendo cha Rais Magufuli cha kupigania maslahi ya wanyonge na kuzuia
kupandisha bei ya umeme nchini.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka wakati wa
kikao cha watumishi wa umoja huo wa kutathmini utendaji kazi wa mwaka
2016 na kuweka utendaji wa mwaka huu.
Shaka
amesema kitendo cha Rais Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesm Mramba, ameonyesha
uzalendo, ujasiri na upendo kwa wananchi ambao walimpa dhamana ya
kuongoza nchi.
“UVCCM
tunaunga mkono uamuzi wa Rais wa kuzuia kupanda kwa bei ya umeme na
ametazama maslahi ya wananchi waliomchagua kuingia madarakani,”amesema
Shaka.
Hata
hivyo, amesema kuwa Tanesco kupitia kwa Mkurugenzi wake Mramba
aliyetumbuliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
waliwaahidi wananchi kutopandisha bei ya umeme.
No comments:
Post a Comment