WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, January 17, 2018

MAAJABU : Apasuka koo kwa kujaribu kuzuia kupiga chafya

Madaktari wa upasuaji wakimuhudumia mgonjwaMadaktari wameonya kwamba kuzuia kupiga chafya kwa kufunga pua na mdomo kunaweza kukusababishia madhara makubwa.
Hii inajiri baada ya madaktari mjini Leicester kumtibu mtu mwenye umri wa miaka 34 ambaye alipusuka koo kwa kujaribu kujizuia kupiga chafya.
Huku kukiwa hakuna nafasi ya hewa ya chafya hiyo kutoka, ililazimika kupasua tishu laini.
Licha ya kwamba kisa hicho sio cha kawaida, madaktari wameonya kwamba watu wengine wanafaa kujua kuhusu hatari hiyo.
Kuzuia kupiga chafya kunaweza kuharibu masikio mbali na kuathiri ubongo wameonya katika jarida la BMJ.

Mtu huyo anasema kuwa alihisi kuwashwa katika koo yake baada ya chafya hiyo na muda mchache baadaye akaanza kuhisi uchungu na akaanza kushindwa kula na kuzungumza.

Wakati madaktari walipomchunguza waligundua kwamba alikuwa ana uvimbe katika koo na shingo yake.
Picha za X ray zilizopigwa zilibaini kwamba kuna hewa inayotoka kupitia tushu laini zilizopasuka kupitia shingo yake.
Mtu huyo alilazimika kulishwa kwa kutumia paipu kwa siku saba mfululilizo ili kutoa fursa kwa tishu hizo kupona.
Baada ya kulazwa hospitalini kwa juma moja, mtu huyo alienda nyumbani ambapo alipona.

KAYOMBO :UBUNGO TUTAJENGA SEKONDARI YA A-LEVEL KUTEKEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM.

ELIMU BURE KWA WOTE: TULIAHIDI TUMETEKELEZA.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo akiwaonyesha utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya ya Ubungo inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Ndg. Lucas Mgonja.

Mkurugenzi Kayombo kwa kushirikiana na watumishi wa Manispaa hiyo ameweza kujenga ukuta (fensi), vyoo na vyumba nane vya madarasa katika shule ya msingi Ubungo Plaza.

Kabla ya hapo shule hiyo ilikuwa haina uzio kitu ambacho kilikuwa ni hatarishi kwa wanafunzi wa jinsia zote.

Pia kulikuwa na uhaba wa vyoo ambapo kilikuwa ni chanzo kikubwa cha magonjwa.

Sambamba na hilo wanafunzi walikuwa wanasoma katika majengo chakavu swala ambalo ni hatarishi kwa maisha yao.

Habari njema ni kuwa Mkurugenzi Kayombo ameahidi kujenga shule ya Sekondari ya A - level katika eneo hilo.

Ujenzi wa sekondari hiyo ya kidato cha tano na sita utasaidia kurahisisha upatikanaji wa elimu katika manispaa hiyo na jambo ambalo litakuwa ni Mara ya kwa Manispaa hiyo tangu ianzishwe.

Jamvi la Hbari linampa Hongera Mkurugenzi Kayombo kwa kuendelea kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 kwa vitendo.

ZIFAHAMU FAIDA MBALIMBALI ZA FENESI KATIKA MWILI WAKO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_CmEdJWjpld8xQfRzwDXKNQo-EURqf7lOdb3hyphenhyphen9c-W7-srTWcUMkP4tEAiNn4oxO76cM-O484_yIXcF4okipP9X1ghKvSGYDYphY0Wa98m3B0AyJd868VKiYtJM5bQ0H7oEjRFky8H-ux/s320/unnamed.pngJ

Huenda umewahi kuliona na kulipita tu ama kutovutiwa na ladha yake ama kukereka na utomvu wake baada ya kula


Habari mbaya kwako ni kwamba umekosa kitu adimu na maridhawa sana......Hili ni moja ya matunda yanayochukuliwa kama MFALME WA MATUNDA (The King of Fruits) kwa kuwa na karibu vitamin vyote muhimu yaani A, B1, B2 na C..



Na sehemu zinazotumika ni majani, matunda, utomvu, mizizi na magamba. Na mfenesi unaweza kukua hadi kufikia kimo cha mita 20.........na nakusihi sana kuanzia leo ujitahidi kula walau punje tatu tu na ukiweza hata mbegu zake kwa kadri ya mada hii



Leo nimejikuta tu nafukunyua tunda hili baada ya kulikuta mahali fulani na jinsi watu walivyokuwa wanatua kilich cha thamani ndipo nilipoanza kugoogle nikakuta faida na hata hilo jina la lugha ya malkia huitwa Jackfruit




Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.



Hakuna anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yake ni katika misitu ya mvua nyingi ya Magharibi ya ghats (western ghats). Lakini kwa sasa inalimwa katika nchi za india, Burma, Sri lanka, China, Malaya, East in indies, Qeens land, Maturities, Hawaii, Suriname, Brazil, Kenya, Uganda na Tanzania, Na nchini Tanzania hulimwa Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na Mbeya(Kyela) nk.




Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuz (fiber) ambazo husaidia kwenye mfumo wa mmeng'enyo na kuchagiza tatizo la kupata haja (constipation) na linasaidia pia kuzuiwa kuvimbiwa.



Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu (cholesterol). Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha,



Sukari ya Fenesi ni dawa ya sukari sumu mwilini kwa kuwa linasharabiwa taratibu mwilini na kufyonza sukari sumu na hii husaidia pia katika kuhibiti shinikizo la damu mwilini ( Jackfruit is more slowly absorbed into the bloodstream, which prevents sugar crashes, sugar cravings, and mood swings, They are well known because of its high potassium content. This helps the blood vessels relax and maintains proper blood pressure.)

kutoka michuzi Blog ambapo tunaambiwa habari hii imeandaliwa na ​ Geofrey Chambua ​kutoka vyanzo mbalimbali

Thursday, January 11, 2018

MKURUGENZI KAYOMBO WA UBUNGO AKABIDHIWA MADARASA YA KIMATAIFA


 
Katika kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha mapinduzi CCM, na kuunga mkono juhudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyejipambanua kuwasimamia na kuwatetea watanzania wanyonge,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John L. Kayombo Aliyesimama

Moja ya Madarasa yaliyopokelewa leo ambayo yametengenezwa pamoja na madawati na miundombinu muhimu ya kusomea wanafunzi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mheshimiwa John Lipesi Kayombo, sambamba na mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Kisare leo wamepokea madarasa mawili yaliyojengwa na wadau wa maendeleo wanaifanya shughuli zao katika manispaa hiyo ya ubungo madarasa yaliyojengwa katika shule ya Sekondari Urafiki iliyopo kata ya Ubungo

madarasa hayo mawili yaliyojengwa kwa ustadi wa aina yake yamejengwa baada ya kukubaliwa kwa maombi ya Mkurugenzi huyo kwa kampuni ya Tanzania Steel Pipes LTD ya jijini hapa na kwamba sehemu kubwa ya madarasa hayo yamejengwa kwa chuma

‘’wakati nateuliwa kuwa mkurugenzi nilifanya ziara kwenye shule hii nilikuta hapa kuna madarasa matano yamechakaa kabisa hayapaswi kutumiwa na wanafunzi wetu, niliagiza mara moja yavunjwe na tutafute pesa kwa ajili ya kujenga madarasa mengine matano mapya…kwa neema ya Mwenyezi Mungu tulikutana na hawa watu wa viwanda tukazungumza nao nikawaomba watujengee madarasa mawili’’. Alisema Mkurugenzi Kayombo wakati akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Ubungo kutoa hotuba ya kuopokea madarasa hayo


‘’niseme tu mheshimiwa mkuu wa wilaya, tutayatunza madarasa haya, ni madarasa ya mfano hayapo wilaya ya ubungo na mkoa wa Dar es salaam hayapo, hapo hapa Urafiki Sekondari’’. Alipngeza Kayombo

kabla ya ujenzi wa madarasa hayo shule hiyo ilikuwa na madarasa matano mabovu yanayohitaji maboresho ambapo baada ya kukamilika kwa madarasa hayo mawili, hivi sasa taratibu za kizabuni kukamilisha ujenzi wa madarasa mengine matatu zimefikia hatua za mwisho na mpaka kufikia mwezi mei mwaka huu inatarajiwa madarasa yote kuwa yamekamilika.




taarifa zaidi kuhusu madarasa hayo tutawaletea.

Tuesday, November 7, 2017

CHADEMA NDUMILAKUWILI :- SAMSON MWIGAMBA

Na. Mwandishi wetu.
 
Kada wa chama cha Mapinduzi CCM ambaye kwa nyakati tofauti amepata kuwa mwenyekiti wa mkoa wa  wa Arusha chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na baadae kutimkia ACT WAZALENDO kuwa muasisi na katibu mkuu wa kwanza wa chama hicho Samson Maingu Mwigamba amewasikitikia watanzania wa vyama vyote wanaohama vyama vyao na kujiunga na CHADEMA na kusema hawana tofauti na mtu anayeruka vumbi na kukanyaga moto na kusisitiza kuwa sifa kuu ya kukuwezesha kuishi kwenye chama hicho ni UNDUMILAKUWILI.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake mkoani Arusha hivi karibuni, mwigamba amesema kwamba chama hicho chake cha awali kimepoteza uwezo wake wa asili wa kujisimamia na hivyo kujikuta kinaenda enda tu sambamba na kusema kuwa chama hicho sio mfano mzuri wa kimbilio la demokrasia na utawala wa sharia unaofuata katiba na usimamizi bora wa fedha akitoa mifano kadhaa.
‘’huwezi hama CCM halafu useme unafuata Demokrasia CHADEMA, utakuwa unachekesha rafiki yangu, pale CHADEMA demokrasia ni Mwenyekiti na mwenyekiti ndio Demokrasia, analotaka ndio huwa na ukijaribu kumkosoa lazima uende na maji’’. Anaanza kueleza Mwigamba

‘’mimi ni kama nimekulia ndani ya Chadema nikishiriki katika nafasi mbalimbali za ndani ya chama, nakuhakikishia kama kuna chama kinasigina katiba basi CHADEMA ni namba moja…kumbuka namna mbowe na wenzake walivyokinyofoa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama ili kimpe yeye nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kudumu, na kumbuka siku tu niliyoanza kuhoji kuhusu hilo nilivyofurumushwa kama kuku pori’’. Anaongeza Mwigamba huku akicheka

Mwigamba anaendele kusema kuwa mara baada ya mbowe kuchukua kijiti cha uenyekiti wa chama hicho alijidhatiti kuhakikisha chama hicho kinakuwa na agenda ya kuisimamia ili kipate kuaminiwa na wananchi na hatimaye kupewa dola jambo ambalo chadema ilifanikiwa kwa kujitanabaisha wazi kuwa wao ni watetezi wa rasilimali za nchi na wapinga ubadhilifu na ain azote za ufisadi.

anasema aliwahi kusimuliwa kisa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe kuhusu chanzo chama hicho kushikilia ajenda ya kupiga vita ufisadi ambapon alimwambia kuwa mwaka 2004 baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti taifa alialikwa kwenye mikutano mikuu ya vyama vya Republican na Democrats vya Marekani alipokutana na Mwanasheria Kivuli aliyetokana na chama cha Democrats wakati huo Republican ikiwa inaongoza nchi chini ya Rais George Bush na mwanasheria huyo  kumweleza Mbowe kwamba haijalishi chama kina sera nzuri kiasi gani, lazima kiaminiwe na wananchi.

http://tabelltz.com/wp-content/uploads/2017/10/samson-mwigamba.jpg 
Samson Mwigamba siku alipojiunga CCM.
 
Aidha mwigamba anasimulia zaidi kuwa  mwanasheria huyo alimweleza mbowe kwamba ameishi Tanzania kwa vipindi tofauti na katika kufanya kazi zake na utafiti aligundua kwamba nchi ilikuwa inapoteza pesa nyingi kupitia ufisadi  na kumwambia Mbowe kwamba kama  nchi ikifanikiwa kuzuia pesa zinazopotea kwa ufisadi, haitahitaji tena kuwa na bajeti tegemezi kwa mataifa ya nje na  kumshauri kuangalia vitabu vya taarifa za Mdhibiti na MKaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anazozitoa kila mwaka ataona pesa nyingi zinavyopotea na  huo ndio ukawa mwanzo wa Mbowe wakati huo akiwa mbunge wa Hai, kuanza kuzunguka mikoani akiambatana na wabunge wengine wa CHADEMA ya wakati huo ambao ni Marehemu Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Dr. Willibrod Slaa (Karatu), Dr. Amani Walid Kabourou (Kigoma mjini) na Grace Kiwelu (Viti maalum) kuelezea mapungufu waliyoyaona wakiwa na ripoti za CAG wakiwaeleza wananchi jinsi ufisadi ulivyokuwa unatafuta mabilioni ya pesa za watanzania maskini.

‘’Huo ndio ukawa mwanzo wa CHADEMA kushikilia ajenda hiyo ya ufisadi mpaka wakaingia nayo kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo Mbowe aligombea urais na kushindwa na Jakaya Kikwete lakini wakapata wabunge watano wa kuchaguliwa na sita wa viti maalum. Ni uchaguzi huo ndio uliowaleta bungeni akina Zitto Kabwe, Halima Mdee na wenzao na hoja ya ufisadi ikawa ni hoja hasa’’. Anaendelea Mwigamba 

Mwigamba anasema kuwa Mbowe alimwambia kwamba waliamua kwenye kamati kuu kwamba kabla ya wabunge wao hawajaenda bungeni, chama kiwe kimefanya utafiti na kuvumbua madudu ya ufisadi ili wanapoenda bungeni wayasimamie hayo na ndio zama zilizoibuka kashfa ambazo majina yake yamebaki kwenye kumbukumbu za watanzania kashfa kama za Meremeta, Deep Green, EPA, Richmond, Buzwagi, na nyinginezo

“Ajenda hiyo ikaipelekea CHADEMA kuwa maarufu sana nchini kiasi cha uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa akagombea urais na kuchuana vikali na Kikwete. Ingawa hakushinda, chama kilichupa kutoka wabunge watano wa majimbo mpaka 23 na baadaye 24, na kutoka wabunge 6 wa viti maalum mpaka 25. Chama kikawa maarufu kiasi cha kufikiriwa kuingia madarakani mwaka 2015. Mbowe alirudia kunihadithia kisa cha huyo mwanasheria kivuli wa kimarekani mara pili tukiwa Karatu mwaka 2012 akitamba juu ya kuutumia vizuri ushauri wa mwanasheria huyo”, anasema Mwigamba.

Mwigamba anasema kwa kipindi kirefu chama hicho kilifanikiwa kujijengea sura ya kuwa watetezi wa Rasilimali za nchi na waoinga ufisadi wakiwa nje lakini wanapokuwa ndani ya chama wanakuwa na madudu makubwa hasa yanayohusu matumizi ya fedha hasa zinazotokana na ruzuku na hivyo kusababisha mitafaruku mikubwa miongoni mwa wananchama na viongozi wao kama ile iliyowahusisha Mbowe na Marehem Chacha Wangwe, na huu wa karibuni baina ya Mbowe na Zitto kabwe ulioishia kwa Zitto kufukuzwa uanachama na hatimaye kutimkia ACT WAZALENDO

“Lakini ndugu mwandishi hebu rejea mwaka 2013 uone Mbowe alivyofanya juhudi kubwa kuvuruga chama kwa matayarisho ya kuja kumpokea yule waliyempachika nembo ya ufisadi. Walianza na Zitto, Kitila na mimi wakamalizia kwa Slaa 2015 na gia ikawa imebadilishiwa angani. Muulize leo Mbowe kuhusu ushauri wa yule mmarekani na wapi wameipotezea ajenda yao ya ufisadi mpaka wananchi wanakosa Imani na chama chao, atakuambia alibadilisha gia angani’’. anasema

‘’alibadilisha gia angani akamchukua Lowassa ambaye Lema alisema kumzomea fisadi kama Lowassa ni heshima kwa Mungu, Msigwa akasema anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili, Lissu akasema CCM wamempa fomu ya kugombea urais fisadi anayetakiwa kuwa gerezani. Leo Nyalandu anaenda kujiunga na chama cha kubadilishia gia angani!!!? ameshajua Mbowe 2020 akibadilisha gia angani ataelekeza wapi chama?” anahoji Mwigamba huku akicheka kwa utani.

‘’huwezi kuwaelewa chadema kama ni popo au ndege, mchana wanasimamia hili, jioni lile basi ilimradi tu…hebu ona mbowe  alivyokuwa anasema Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA…leo amebanwa nayeye kwenye madili yake amegeuka anasema Magufuli dikteta/…hakuna Dikteta katika siasa za Tanzania kumzidi Mbowe nakuambia mimi, chadema wanalijua hilo na UKAWA halikadharika’’.

‘’akigeuka huku anaona waliojihusisha na ufisadi wanapukutishwa kutoka serikalini, akigeuka anaona utumishi wa umma unavyorejea kwenye uadilifu na uchapakazi, miradi ya maji inatekelezwa hata iliyolala kwa miaka, miradi ya barabara za juu iliyohubiriwa kwa miaka inaanza, reli ya standard gauge iliyoishia kusemwa midomoni kwa karne inanyanyuka, miradi ya umeme, nk, akaona hapo hana jinsi, akasema rais anatekeleza ilani ya CHADEMA’’. Anaendelea Mwigamba

‘’ Mbowe na CHADEMA yake walipoona rais anawashughulikia mpaka wale waliowachangia wao pesa za kampeni na hatimaye kumgusa Mbowe mwenyewe kwa ufisadi mkubwa aliolifanyia shirika la nyumba la taifa kwa makumi ya miaka, hali yao ikawa ngumu vijana wa mtaani wanasema siku hizi vyuma vikakaza, wakaanza kusema rais anavunja sheria na hatimaye wakaibuka na udikteta’’. Mwigamba anaongeza  
Tukio jingine alilolibainisha Mwigamba ni la Waziri Mkuu wa zamani Fredrick  Sumaye.

’’ Ni Sumaye huyu huyu aliyeshambuliwa sana na Mbowe na CHADEMA yake miaka ya 2000 pale wafanyabiashara wasio wana CCM walipolalamika kunyanyaswa na mamlaka ya serikali hususani TRA. Sumaye akaibuka na kusema,…. Kama mfanyabiashara unataka mambo yako yakunyookee, tundika bendera ya CCM kwenye biashara yako…. Walimtukana Sumaye kila matusi na kuonyesha anavyotumia vibaya madaraka ya uwaziri mkuu lakini leo Sumaye ni nguzo kuu kwenye CHADEMA’’.

‘’Hauwezi kuwa na akili timamu halafu uwaamini chadema si unakumbuka  Kwenye uchaguzi wa 2015 kimsingi Sumaye ndiye alikuwa mpiga zumari mkuu na sasa ni mmoja wa watu wanaopigiwa upatu ndani ya CHADEMA kugombea urais 2020 mtu aliyekaa kwenye uwaziri mkuu kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote lakini anayeongoza kwa kukosa alama hata moja aliyoiacha eti leo agombee urais!!!? Hiyo ndiyo CHADEMA’’. Anazidi kueleza

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxqWarFaY9e3tI45e4vPlfuzK5ix-C2XhnJNvfKPpi9r1kCsag1BdAVCJ5l_HfpLVAduniPaYvy0HbEK2sYTTxZmoZ2Pe_kAh4Bjtr5Y_GW_Iy9mBBlBXNJKLMIsN5XUF7g4eC6ibmEjA/s1600/IMG-20150727-WA0027.jpg
“Mtazame hata huyuNyalandu mwenyewe. Angalia clip ya video ya Joshua Nassari bungeni, angalia tweets za Mch. Msigwa na Halima Mdee. Hivi hawaoni hata aibu mtu ambaye haijapita hata miaka mitatu tangu mmwite majina ya kila aina (mshika makalio ya mabinti askari wa wanyamapori, mtalii wa kutumbua kodi za watanzania na wasanii Marekani, fisadi wa hati za rais za uwindaji, nk) leo mnamwita kamanda, jembe, mara dume, mmh!”

Mwigamba anawapa pole sana wale wote wanaokimbilia CHADEMA na wale wanaojiandaa kufanya hivyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020.

''Kama ni mafisadi waende maana kwenye seerikali ya Magufuli hamna namna ya fisadi kusurvive. Ni sawa na kumwambia mwenye dhambi asurvive mbele ya nuru ya Mwenyezi Mungu. Haiwezekani. Wa namna hiyo watangulie tu CHADEMA ndiko kwenye ngome mpya ya mafisadi. Lakini wale walio waadilifu wanaodhani kule ni kimbilio, wamuulize Dr. Slaa atawasimulia vizuri zaidi. CHADEMA mchana unaweza kuwaona malaika safi toka mbinguni na usiku ukakuta ni mashetani wenye mapembe kabisa!''. alimalizia