Na. Mwandishi wetu.
Kada wa chama cha Mapinduzi CCM ambaye kwa nyakati
tofauti amepata kuwa mwenyekiti wa mkoa wa wa Arusha chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA na baadae kutimkia ACT WAZALENDO kuwa muasisi na katibu mkuu wa kwanza
wa chama hicho Samson Maingu Mwigamba amewasikitikia watanzania wa vyama vyote
wanaohama vyama vyao na kujiunga na CHADEMA na kusema hawana tofauti na mtu
anayeruka vumbi na kukanyaga moto na kusisitiza kuwa sifa kuu ya kukuwezesha
kuishi kwenye chama hicho ni UNDUMILAKUWILI.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum
yaliyofanyika nyumbani kwake mkoani Arusha hivi karibuni, mwigamba amesema
kwamba chama hicho chake cha awali kimepoteza uwezo wake wa asili wa
kujisimamia na hivyo kujikuta kinaenda enda tu sambamba na kusema kuwa chama
hicho sio mfano mzuri wa kimbilio la demokrasia na utawala wa sharia unaofuata
katiba na usimamizi bora wa fedha akitoa mifano kadhaa.
‘’huwezi hama CCM halafu useme unafuata Demokrasia
CHADEMA, utakuwa unachekesha rafiki yangu, pale CHADEMA demokrasia ni
Mwenyekiti na mwenyekiti ndio Demokrasia, analotaka ndio huwa na ukijaribu
kumkosoa lazima uende na maji’’. Anaanza kueleza Mwigamba
‘’mimi ni kama nimekulia ndani ya Chadema nikishiriki
katika nafasi mbalimbali za ndani ya chama, nakuhakikishia kama kuna chama
kinasigina katiba basi CHADEMA ni namba moja…kumbuka namna mbowe na wenzake
walivyokinyofoa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama ili
kimpe yeye nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kudumu, na kumbuka siku tu niliyoanza
kuhoji kuhusu hilo nilivyofurumushwa kama kuku pori’’. Anaongeza Mwigamba huku
akicheka
Mwigamba anaendele kusema kuwa mara baada ya mbowe
kuchukua kijiti cha uenyekiti wa chama hicho alijidhatiti kuhakikisha chama
hicho kinakuwa na agenda ya kuisimamia ili kipate kuaminiwa na wananchi na
hatimaye kupewa dola jambo ambalo chadema ilifanikiwa kwa kujitanabaisha wazi
kuwa wao ni watetezi wa rasilimali za nchi na wapinga ubadhilifu na ain azote za
ufisadi.
anasema aliwahi kusimuliwa kisa na Mwenyekiti wa
CHADEMA Taifa Freeman Mbowe kuhusu chanzo chama hicho kushikilia ajenda ya
kupiga vita ufisadi ambapon alimwambia kuwa mwaka 2004 baada ya kuchaguliwa
kuwa mwenyekiti taifa alialikwa kwenye mikutano mikuu ya vyama vya Republican
na Democrats vya Marekani alipokutana na Mwanasheria Kivuli aliyetokana na
chama cha Democrats wakati huo Republican ikiwa inaongoza nchi chini ya Rais
George Bush na mwanasheria huyo kumweleza
Mbowe kwamba haijalishi chama kina sera nzuri kiasi gani, lazima kiaminiwe na
wananchi.
Samson Mwigamba siku alipojiunga CCM.
Aidha mwigamba anasimulia zaidi kuwa mwanasheria huyo alimweleza mbowe kwamba ameishi
Tanzania kwa vipindi tofauti na katika kufanya kazi zake na utafiti aligundua
kwamba nchi ilikuwa inapoteza pesa nyingi kupitia ufisadi na kumwambia Mbowe kwamba kama nchi ikifanikiwa kuzuia pesa zinazopotea kwa ufisadi,
haitahitaji tena kuwa na bajeti tegemezi kwa mataifa ya nje na kumshauri kuangalia vitabu vya taarifa za
Mdhibiti na MKaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anazozitoa kila mwaka ataona
pesa nyingi zinavyopotea na huo ndio ukawa
mwanzo wa Mbowe wakati huo akiwa mbunge wa Hai, kuanza kuzunguka mikoani
akiambatana na wabunge wengine wa CHADEMA ya wakati huo ambao ni Marehemu
Philemon Ndesamburo (Moshi mjini), Dr. Willibrod Slaa (Karatu), Dr. Amani Walid
Kabourou (Kigoma mjini) na Grace Kiwelu (Viti maalum) kuelezea mapungufu
waliyoyaona wakiwa na ripoti za CAG wakiwaeleza wananchi jinsi ufisadi
ulivyokuwa unatafuta mabilioni ya pesa za watanzania maskini.
‘’Huo ndio ukawa mwanzo wa CHADEMA kushikilia ajenda
hiyo ya ufisadi mpaka wakaingia nayo kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo Mbowe
aligombea urais na kushindwa na Jakaya Kikwete lakini wakapata wabunge watano
wa kuchaguliwa na sita wa viti maalum. Ni uchaguzi huo ndio uliowaleta bungeni
akina Zitto Kabwe, Halima Mdee na wenzao na hoja ya ufisadi ikawa ni hoja hasa’’.
Anaendelea Mwigamba
Mwigamba anasema kuwa Mbowe alimwambia kwamba waliamua
kwenye kamati kuu kwamba kabla ya wabunge wao hawajaenda bungeni, chama kiwe kimefanya
utafiti na kuvumbua madudu ya ufisadi ili wanapoenda bungeni wayasimamie hayo
na ndio zama zilizoibuka kashfa ambazo majina yake yamebaki kwenye kumbukumbu
za watanzania kashfa kama za Meremeta, Deep Green, EPA, Richmond, Buzwagi, na nyinginezo
“Ajenda hiyo ikaipelekea CHADEMA kuwa maarufu sana
nchini kiasi cha uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa akagombea urais na kuchuana
vikali na Kikwete. Ingawa hakushinda, chama kilichupa kutoka wabunge watano wa
majimbo mpaka 23 na baadaye 24, na kutoka wabunge 6 wa viti maalum mpaka 25.
Chama kikawa maarufu kiasi cha kufikiriwa kuingia madarakani mwaka 2015. Mbowe
alirudia kunihadithia kisa cha huyo mwanasheria kivuli wa kimarekani mara pili
tukiwa Karatu mwaka 2012 akitamba juu ya kuutumia vizuri ushauri wa mwanasheria
huyo”, anasema Mwigamba.
Mwigamba anasema kwa kipindi kirefu chama hicho
kilifanikiwa kujijengea sura ya kuwa watetezi wa Rasilimali za nchi na waoinga
ufisadi wakiwa nje lakini wanapokuwa ndani ya chama wanakuwa na madudu makubwa
hasa yanayohusu matumizi ya fedha hasa zinazotokana na ruzuku na hivyo kusababisha
mitafaruku mikubwa miongoni mwa wananchama na viongozi wao kama ile
iliyowahusisha Mbowe na Marehem Chacha Wangwe, na huu wa karibuni baina ya
Mbowe na Zitto kabwe ulioishia kwa Zitto kufukuzwa uanachama na hatimaye
kutimkia ACT WAZALENDO
“Lakini ndugu mwandishi hebu rejea mwaka 2013 uone
Mbowe alivyofanya juhudi kubwa kuvuruga chama kwa matayarisho ya kuja kumpokea
yule waliyempachika nembo ya ufisadi. Walianza na Zitto, Kitila na mimi
wakamalizia kwa Slaa 2015 na gia ikawa imebadilishiwa angani. Muulize leo Mbowe
kuhusu ushauri wa yule mmarekani na wapi wameipotezea ajenda yao ya ufisadi
mpaka wananchi wanakosa Imani na chama chao, atakuambia alibadilisha gia angani’’.
anasema
‘’alibadilisha gia angani akamchukua Lowassa ambaye
Lema alisema kumzomea fisadi kama Lowassa ni heshima kwa Mungu, Msigwa akasema
anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili, Lissu akasema CCM wamempa fomu ya
kugombea urais fisadi anayetakiwa kuwa gerezani. Leo Nyalandu anaenda kujiunga
na chama cha kubadilishia gia angani!!!? ameshajua Mbowe 2020 akibadilisha gia
angani ataelekeza wapi chama?” anahoji Mwigamba huku akicheka kwa utani.
‘’huwezi kuwaelewa chadema kama ni popo au ndege,
mchana wanasimamia hili, jioni lile basi ilimradi tu…hebu ona mbowe alivyokuwa anasema Magufuli anatekeleza ilani
ya CHADEMA…leo amebanwa nayeye kwenye madili yake amegeuka anasema Magufuli dikteta/…hakuna
Dikteta katika siasa za Tanzania kumzidi Mbowe nakuambia mimi, chadema wanalijua
hilo na UKAWA halikadharika’’.
‘’akigeuka huku anaona waliojihusisha na ufisadi
wanapukutishwa kutoka serikalini, akigeuka anaona utumishi wa umma unavyorejea
kwenye uadilifu na uchapakazi, miradi ya maji inatekelezwa hata iliyolala kwa
miaka, miradi ya barabara za juu iliyohubiriwa kwa miaka inaanza, reli ya
standard gauge iliyoishia kusemwa midomoni kwa karne inanyanyuka, miradi ya
umeme, nk, akaona hapo hana jinsi, akasema rais anatekeleza ilani ya CHADEMA’’.
Anaendelea Mwigamba
‘’ Mbowe na CHADEMA yake walipoona rais
anawashughulikia mpaka wale waliowachangia wao pesa za kampeni na hatimaye
kumgusa Mbowe mwenyewe kwa ufisadi mkubwa aliolifanyia shirika la nyumba la
taifa kwa makumi ya miaka, hali yao ikawa ngumu vijana wa mtaani wanasema siku
hizi vyuma vikakaza, wakaanza kusema rais anavunja sheria na hatimaye wakaibuka
na udikteta’’. Mwigamba anaongeza
Tukio jingine alilolibainisha Mwigamba ni la Waziri
Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye.
’’ Ni Sumaye huyu huyu aliyeshambuliwa sana na Mbowe
na CHADEMA yake miaka ya 2000 pale wafanyabiashara wasio wana CCM
walipolalamika kunyanyaswa na mamlaka ya serikali hususani TRA. Sumaye akaibuka
na kusema,…. Kama mfanyabiashara unataka mambo yako yakunyookee, tundika
bendera ya CCM kwenye biashara yako…. Walimtukana Sumaye kila matusi na
kuonyesha anavyotumia vibaya madaraka ya uwaziri mkuu lakini leo Sumaye ni
nguzo kuu kwenye CHADEMA’’.
‘’Hauwezi kuwa na akili timamu halafu uwaamini chadema
si unakumbuka Kwenye uchaguzi wa 2015
kimsingi Sumaye ndiye alikuwa mpiga zumari mkuu na sasa ni mmoja wa watu
wanaopigiwa upatu ndani ya CHADEMA kugombea urais 2020 mtu aliyekaa kwenye
uwaziri mkuu kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote lakini anayeongoza kwa
kukosa alama hata moja aliyoiacha eti leo agombee urais!!!? Hiyo ndiyo CHADEMA’’.
Anazidi kueleza
“Mtazame hata huyuNyalandu mwenyewe. Angalia clip ya
video ya Joshua Nassari bungeni, angalia tweets za Mch. Msigwa na Halima Mdee.
Hivi hawaoni hata aibu mtu ambaye haijapita hata miaka mitatu tangu mmwite
majina ya kila aina (mshika makalio ya mabinti askari wa wanyamapori, mtalii wa
kutumbua kodi za watanzania na wasanii Marekani, fisadi wa hati za rais za
uwindaji, nk) leo mnamwita kamanda, jembe, mara dume, mmh!”
Mwigamba anawapa pole sana wale wote wanaokimbilia
CHADEMA na wale wanaojiandaa kufanya hivyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020.
No comments:
Post a Comment